title : WAZIRI LUKUVI AAGIZA WALIOPOTOSHA MIPAKA YA KIJIJI CHA MABWEGERE KILOSA WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA
kiungo : WAZIRI LUKUVI AAGIZA WALIOPOTOSHA MIPAKA YA KIJIJI CHA MABWEGERE KILOSA WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA
WAZIRI LUKUVI AAGIZA WALIOPOTOSHA MIPAKA YA KIJIJI CHA MABWEGERE KILOSA WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA
Na Munir Shemweta, Morogoro
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amekabidhi taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji saba vya wilaya hiyo na mpango wa utekelezaji wake na kuagiza wote waliohusika kupotosha mipaka ya eneo hilo akiwemo Mkurugenzi Msaidizi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi kuchukuliwa hatua za kisheria.
Lukuvi alitoa agizo hilo leo mkoani Morogoro wakati akikabidhi taarifa ya uchunguzi iliyofanywa na Jaji wa Mahakama Kuu ambaye sasa ni jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacob Mwambegele kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe kuhusiana na mgogoro wa mipaka ya kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani vya Mambegwa, Mbigiri, Dumila, Matongolo na Mfulu vilivyopo Wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro.
“Wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika process yote ambayo kwa kiasi fulani imeigharimu serikali fedha nyingi na kuipa maumivu serikali katika suala hilo ni lazima wachukuliwe hatua kali” alisema Lukuvi.
Taarifa ya uchunguzi ilibaini chanzo cha mgogoro ni kukosekana ushirikishwaji wa vijiji jirani katika kuainisha na kuweka mipaka ya kijiji cha Mabwegere jambo lililosababisha kijiji kiwe na eneo la ukubwa wa hekta 10, 234 kuliko hata kijiji mama cha Mfulu chenye hekta 1,717 jambo lililothibitishwa na ukweli kwamba mipaka ya kijiji hicho imeingia ndani ya mipaka ya kata tatu za Mbigiri, Msowero, na Kitete ingawa kiutawala kijiji cha Mabwegere kinaratibiwa na kata ya Kitete.
Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiangalia taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro kabla ya kuikabidhi taarifa hiyo kwa mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (kulia). Wengine katika picha Naibu Waziri TAMISEMI Joseph Kakunda (wa pili kushoto) na kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo Bi. Merry Mwanjelwa.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na viongozi wa mkoa wa Morogoro pamoja na watendaji wa Wilaya ya Kilosa wakati wa kukabidhi taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro. kulia ni mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe. Wengine katika picha wa pili kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI Joseph Kakunda na kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo Bi. Merry Mwanjelwa.
Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro. Kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI Joseph Kakunda.
aadhi ya viongozi wa halmashauri za vijiji saba wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati wa kuwapa taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro.
Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na viongozi wa halmashauri za vijiji saba kuhusu taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro.

Hivyo makala WAZIRI LUKUVI AAGIZA WALIOPOTOSHA MIPAKA YA KIJIJI CHA MABWEGERE KILOSA WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA
yaani makala yote WAZIRI LUKUVI AAGIZA WALIOPOTOSHA MIPAKA YA KIJIJI CHA MABWEGERE KILOSA WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI LUKUVI AAGIZA WALIOPOTOSHA MIPAKA YA KIJIJI CHA MABWEGERE KILOSA WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/waziri-lukuvi-aagiza-waliopotosha.html
0 Response to "WAZIRI LUKUVI AAGIZA WALIOPOTOSHA MIPAKA YA KIJIJI CHA MABWEGERE KILOSA WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA"
Post a Comment