title : WAKAZI WA MUHEZA WAITIKIA WITO KWA KUJENGA VYOO BORA
kiungo : WAKAZI WA MUHEZA WAITIKIA WITO KWA KUJENGA VYOO BORA
WAKAZI WA MUHEZA WAITIKIA WITO KWA KUJENGA VYOO BORA
Na Humphrey Shao, Muheza Tanga
MSANII wa Muziki wa Kughani , Mrisho Mpoto alimaharufu kama Mjomba amesema kuwa kampeni ya Nyumba ni Choo inayoendelea katika Wilaya ya Muheza imeweza kuja na Matokeo mazuri ya awali kwa wakazi wa eneo hilo kuweka mahadhimio ya kujenga vyoo bora.
Mrisho Mpoto amesema kuwa wakati wanafika katika Wilaya hiyo walijua itakuwa ni ngumu lakini cha ajabu wakati wanatoa somo la kwanza tu wakazi hao wamehazimia kujengwa vyoo kabla ya kukamilika kwa mradi.
"wakazi wa Muheza wamehazimia kujenga vyoo bora kwa kukubali kauli mbiu yetu kuwa nyumba ni choo hivyo kwasasa wanamiminika uwanjani kwa ajili ya kujifunza namna ya kujenga kuta nne za Choo Bora" amesema Mrisho .
Mpoto amemaliza kwa kuwataka watanzania kuweka kipaumbele katika ujenzi wa vyoo bora ambavyo vitachangia kupunguza magonjwa ya kuambukiza yatokanayo na uchafu kama kuhara na kipindupindu
Msanii wa Muziki wa Kughani, Mrisho Mpoto akitumbuiz akatika kampeni ya Nyumba ni Choo Katika Wilaya ya Wizara ya Afya Wilaya Muheza mkoani Tanga ambapo watu wameweza kuitikia wito wa kampeni hiyo na kujiwekea mahazimio ya kujenga vyoo bora kabla ya kukamilika kwa kampeni hiyo
Wakazi wa Wilaya ya Muheza wakifatilia kampeni ya Nyumba ni Choo inayoendeshwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Mjomba Bendi
Wacheza Sarakakasi wa kundi la Mjomba Theatre wakionyesha mchezo wa Sarakasi wa kuhamasisha ujenzi wa Vyoo bora kwa kauli ya Nyumba ni Choo kwa wakazi wa Muheza.
Burudani ikiendelea
Hivyo makala WAKAZI WA MUHEZA WAITIKIA WITO KWA KUJENGA VYOO BORA
yaani makala yote WAKAZI WA MUHEZA WAITIKIA WITO KWA KUJENGA VYOO BORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKAZI WA MUHEZA WAITIKIA WITO KWA KUJENGA VYOO BORA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/wakazi-wa-muheza-waitikia-wito-kwa.html
0 Response to "WAKAZI WA MUHEZA WAITIKIA WITO KWA KUJENGA VYOO BORA"
Post a Comment