MKURUGENZI MTENDAJI WA MIGODI YA PANGEA,NORTH MARA, BULYANHULU KIZIMBANI KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR

MKURUGENZI MTENDAJI WA MIGODI YA PANGEA,NORTH MARA, BULYANHULU KIZIMBANI KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MKURUGENZI MTENDAJI WA MIGODI YA PANGEA,NORTH MARA, BULYANHULU KIZIMBANI KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MKURUGENZI MTENDAJI WA MIGODI YA PANGEA,NORTH MARA, BULYANHULU KIZIMBANI KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR
kiungo : MKURUGENZI MTENDAJI WA MIGODI YA PANGEA,NORTH MARA, BULYANHULU KIZIMBANI KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR

soma pia


MKURUGENZI MTENDAJI WA MIGODI YA PANGEA,NORTH MARA, BULYANHULU KIZIMBANI KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
MKURUGENZI mtendaji  migodi wa Pangea, North Mara na Bulyanhulu, ASA Mbulaja Mwaipopo, leo Novemba 23.2018 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka tisa likiwemo la kutakatisha zaidi ya USD milioni Tisa.

Mshtakiwa Mwaipopo ambaye pia ni mhandisi wa madini amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu  Mkazi  Mfawidhi,  Kevin Mhina na Jopo la mawakili watatu waliokuwa wakiongozwa na wakili  wa  serikali  Mkuu,  Faraja  Nchimbi  akisaidiana na Wakili wa serikali Mwandamizi,  Mutalemwa Kishenyi na Jackilline Nyantori. 

Mbali na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo yako manne, Mwaipopo pia anashtakiwa na shtaka moja la kula njama, shtaka moja la kuongoza kutendeka kwa uhalifu, shtaka moja la kughushi, mashtaka mawili ya kukwepa kodi.

Mshtakiwa Mwaipopo anatarajiwa kuunganishwa na washtakiwa wenzake ambao ni Rais wa zamani wa migodi hiyo,  Deogratias Mwanyika na Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu Alex Lugendo ambao mwisho mwa wiki iliyopita  (Oktoba 17.2018) walisomewa mashtaka 39, yakiwemo hayo Tisa aliyosomewa Mwaipopo leo, yakiwemo pia ya utakatishaji na kukwepa kodi zaidi ya USD milioni 112.

Mbali na Mwanyika, Lugendo na Mwaipopo washtakiwa wengine ni kampuni ya Mgodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu

Akisoma hati ya mashtaka dhidi ya Mwaipopo wakili Nchimbi amedai, washtakiwa hao pamoja na watu wengine ambao bado hawajakamatwa, walitenda makosa hayo kati ya Aprili 11.2008 na June 30.2007 katika sehemu tofauti za jiji la dar es Salaam, Kahama Mkoani Shinyanga, Tarime Mara, Biharamulo Kagera maeneo ambayo yapo katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo katika mji wa Johannesburg, Afrika Kusini, Toronto Canada na nchini  Uingereza.

Imedaiwa katika kipindi hicho na mahali hapo Mwaipopo na wenzake, pamoja na watu wengine ambao bado hawajakamatwa walikula njama ya ya kutenda makosa ya kughushi na ukwepaji wa Kodi.

Pia mshtakiwa anadaiwa kutoa msaada katika kusimamia mkakati wa kihalifu kwa nia ya kupata faida.

 Aidha mshtakiwa Mwaipopo na wenzake,wadaiwa kati ya Mei 16.2008 na Desemba 31,2008 huko Kahama na Biaramulo, walitoa tamko la uongo kwa kamishna Generali wa  TRA kwa nia ya kukwepa kodi kulipa USD 9,309,600 ambayo ilikuwa ni kodi iliyopaswa kulipwa kwa TRA.

Katika shtaka la kughushi washtakiwa hao wakiwa na nia ya ulaghai waligushi mkataba wa mkopo wakitaka kuonyesha kwamba Aprili 30.2014 Kampuni ya Pangea limited ilikubali kukopa USD 90,000,000 ikiwa na riba Kutoka benki ya kimataifa ya barrick huku wakijua kuwa siyo kweli.


 Hata hivyo wa mshtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika. Na kesi itatajwa tena ktoba 31, mwaka huu ambao Mshtakiwa Mwaipopo ataunganishwa na wenzake


Mkurugenzi mtendaji  migodi wa Pangea, North Mara na Bulyanhulu, ASA Mbulaja Mwaipopo,leo Novemba 23.2018 akiingia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashtaka tisa likiwemo la kutakatisha zaidi ya USD milioni Tisa.


Hivyo makala MKURUGENZI MTENDAJI WA MIGODI YA PANGEA,NORTH MARA, BULYANHULU KIZIMBANI KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR

yaani makala yote MKURUGENZI MTENDAJI WA MIGODI YA PANGEA,NORTH MARA, BULYANHULU KIZIMBANI KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MKURUGENZI MTENDAJI WA MIGODI YA PANGEA,NORTH MARA, BULYANHULU KIZIMBANI KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/mkurugenzi-mtendaji-wa-migodi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MKURUGENZI MTENDAJI WA MIGODI YA PANGEA,NORTH MARA, BULYANHULU KIZIMBANI KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR"

Post a Comment