title : Muhimbili Waungana na Watanzania Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwa kutembelea Butiama
kiungo : Muhimbili Waungana na Watanzania Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwa kutembelea Butiama
Muhimbili Waungana na Watanzania Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwa kutembelea Butiama
Wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) walioko Hospitali ya Rufaa Musoma mkoani Mara wameungana na Watanzania kuazimisha kumbukizi ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Butiama mkoani Mara.
Wataalam hao wametembelea Kijiji cha Mwitongo ambako mwili wa Mwalimu Nyerere omehifadhiwa na kupatiwa maelezo mbalimbali kuhusu histoaria yake.
Katika maadhimisho hayo wananchi mbalimbali wamejitokeza wakiwamo wanafunzi, watalam wa afya Muhimbili na kufanyika kwa ibaada ya kumuombea Baba wa Taifa.
Baada ya wataalam hao kushiriki kwenye kumbukizi ya Hayati Mwalimu Nyerere leo, kesho Jumatatu (tarehe 15, 2018) wanaendelea kutoa huduma mbalimbali matibabu kwa wakazi wa mkoa huo na mikoa ya jirani kwa njia ya mkoba pamoja na kujenga uwezo kwa wataalamu wa Hospitali ya Rufaa ya Musoma.
Mwalimu Nyerere alifariki dunia Oktoba 14, mwaka 1999 katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas nchini Uingereza ambako alikwenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Madaktari walieleza kwamba kifo chake kilisababishwa na ugonjwa wa saratani ya damu.
Oktoba 14 kila mwaka imefanywa kuwa siku maalam ya kitaifa ili kutoa nafasi ya kumkumbuka na kutafakari mema na mazuri aliyoyafanya enzi za uhai wake.
Wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Hospitali ya Rufaa ya Musoma wakiwa katika kaburi la Baba wa Taifa baada ya kumuombea leo ikiwa ni siku ya kumbikizi yake ambayo hufanyika Oktoba 14 kila mwaka.
Baadhi ya wataalam wa Hospitali ya Rufaa Musoma na Muhimbili wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuelekea kwenye nyumba ambako Baba wa Taifa alikuwa akipumzika enzi za uhai wake na wakati mwingine kukutana na wageni wake.
Wataalam wakiwa katika sebule ambako Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa akipumzika na Mama Nyerere.
Jengo la Makumbusho ya Hayati Mwalimu Nyerere.
Dkt. Brighton Mushengezi akipitia historia katika Makumbusho ya Hayati Mwalimu Nyerere yaliopo kwenye Kijiji cha Mwitongo, Butiama mkoani Mara.
Hivyo makala Muhimbili Waungana na Watanzania Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwa kutembelea Butiama
yaani makala yote Muhimbili Waungana na Watanzania Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwa kutembelea Butiama Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Muhimbili Waungana na Watanzania Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwa kutembelea Butiama mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/muhimbili-waungana-na-watanzania.html
0 Response to "Muhimbili Waungana na Watanzania Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwa kutembelea Butiama"
Post a Comment