title : LUGOLA: SERIKALI ITAWASHUGHULIKIA VIONGOZI WA DINI WALIOJIPENYEZA KUANZISHA MAKANISA NA MISIKITI KWA LENGO LA KUFANYA UCHOCHEZI, KUVURUGA AMANI NCHINI
kiungo : LUGOLA: SERIKALI ITAWASHUGHULIKIA VIONGOZI WA DINI WALIOJIPENYEZA KUANZISHA MAKANISA NA MISIKITI KWA LENGO LA KUFANYA UCHOCHEZI, KUVURUGA AMANI NCHINI
LUGOLA: SERIKALI ITAWASHUGHULIKIA VIONGOZI WA DINI WALIOJIPENYEZA KUANZISHA MAKANISA NA MISIKITI KWA LENGO LA KUFANYA UCHOCHEZI, KUVURUGA AMANI NCHINI
Na Felix Mwagara, MOHA-Ngara.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema baadhi ya viongozi wa dini nchini wamejipenyeza na kuanzisha makanisa na misikiti kwa lengo la kuanzisha vichaka vya kujificha ili tujue ni watu wa Mungu kumbe wanataka kufanya uchochezi na kuvuruga amani nchini.
Lugola amesema Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli haitawavumilia wale wote walioanzisha taasisi hizo kwa lengo lao binafsi na itahakikisha inawashughulikia ipasavyo bila kuwaonea huruma.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa Mji wa Ngara, leo, Lugola amesema makanisa na misikiti ambayo imesajiliwa na Wizara yake hatakubali kuona viongozi hao ambao wanajifanya kuwa na watu wa Mungu kumbe wanamalengo hayo binafsi.
“Makanisa na miskiti itakayobainika ina malengo hayo, sitaona haya kuifutia usajili, na pia nawataka viongozi wa dini endapo migogoro inaibuka hakikisheni mnaitatua wenyewe kwa amani,” alisema Lugola.
Lugola ameongeza kuwa, Serikali inaheshimu imani ya dini na pia viongozi wao wanamchango mkubwa katika maendeleo ya nchi kutokakana na maombi pamoja na kuwaongoza waumini wao vizuri, lakini pia wapo baadhi ya viongozi hao wa dini, wanaingiza masuala ya siasa makanisani na misikitini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa Mji wa Ngara, Mkoani Kagera (hawapo pichani), katika Mkutano wa hadhara uliofanyika mjini humo, leo. Katika mkutano huo, Lugola amesema baadhi ya viongozi wa dini nchini wamejipenyeza na kuanzisha makanisa na misikiti kwa lengo la kuanzisha vichaka vya kujificha ili tujue ni watu wa Mungu kumbe wanataka kufanya uchochezi na kuvuruga amani nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na Askari na Watumishi wa Wizara yake wa Wilaya ya Ngara, Mkoani Kagera (hawapo pichani), katika kikao hicho, Lugola aliwataka watumishi hao wafanye kazi kwa kujituma bila kuchukua rushwa. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Luten Kanali Michael Mtenjele. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi.
Baadhi ya Askari na Watumishi wa Mjini Ngara, Mkoani Kagera wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani) wakati alipokua anajibu maswali ya watumishi hao kuhusu masuala mbalimbali ya Wizara yake, katika kikao kilichofanyika mjini humo, leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala LUGOLA: SERIKALI ITAWASHUGHULIKIA VIONGOZI WA DINI WALIOJIPENYEZA KUANZISHA MAKANISA NA MISIKITI KWA LENGO LA KUFANYA UCHOCHEZI, KUVURUGA AMANI NCHINI
yaani makala yote LUGOLA: SERIKALI ITAWASHUGHULIKIA VIONGOZI WA DINI WALIOJIPENYEZA KUANZISHA MAKANISA NA MISIKITI KWA LENGO LA KUFANYA UCHOCHEZI, KUVURUGA AMANI NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala LUGOLA: SERIKALI ITAWASHUGHULIKIA VIONGOZI WA DINI WALIOJIPENYEZA KUANZISHA MAKANISA NA MISIKITI KWA LENGO LA KUFANYA UCHOCHEZI, KUVURUGA AMANI NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/lugola-serikali-itawashughulikia.html
0 Response to "LUGOLA: SERIKALI ITAWASHUGHULIKIA VIONGOZI WA DINI WALIOJIPENYEZA KUANZISHA MAKANISA NA MISIKITI KWA LENGO LA KUFANYA UCHOCHEZI, KUVURUGA AMANI NCHINI"
Post a Comment