DC Kinondoni aahidi kutatua kero ya barabara inayokwenda Kliniki ya Heameda, Mengi ashangazwa na maajabu ya Dk.Mwandolela

DC Kinondoni aahidi kutatua kero ya barabara inayokwenda Kliniki ya Heameda, Mengi ashangazwa na maajabu ya Dk.Mwandolela - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC Kinondoni aahidi kutatua kero ya barabara inayokwenda Kliniki ya Heameda, Mengi ashangazwa na maajabu ya Dk.Mwandolela, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC Kinondoni aahidi kutatua kero ya barabara inayokwenda Kliniki ya Heameda, Mengi ashangazwa na maajabu ya Dk.Mwandolela
kiungo : DC Kinondoni aahidi kutatua kero ya barabara inayokwenda Kliniki ya Heameda, Mengi ashangazwa na maajabu ya Dk.Mwandolela

soma pia


DC Kinondoni aahidi kutatua kero ya barabara inayokwenda Kliniki ya Heameda, Mengi ashangazwa na maajabu ya Dk.Mwandolela


VIONGOZI wa ngazi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es  Salaam wamepongeza uongozi wa Kliniki ya Heameda iliyopo Bunju B ambayo imekuwa ikitoa huduma za matibabu ya moyo kwa wananchi wa wilaya hiyo na maeneo mengine huku ukiahidi kushughulikia kero ya ubovu  barabara inayoelekea kwenye kliniki hiyo ambayo imetajwa kutoa mchango mkubwa kuokoa maisha ya Watanzania.

Hayo yamesemwa jana na ujumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni kupitia Mkuu wake wa Wilaya Daniel  Chongolo na Mganga Mkuu wa halmashauri hiyo Dk.Christowell Mande wakati wa uzinduzi rasmi wa Kliniki ya Heameda ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP Reginald Mengi.

Akizungumzia Kliniki hiyo Chongolo amesema Serikali inathamini mchango wa kliniki hiyo kwa kutoa huduma kwa wananchi wa Kinondoni na hasa walioko maeneo hayo ambayo hayana vituo vingi vya afya.Pia amejibu kuhusu ombi kero ya barabara inayoingia kwenye  kliniki hiyo kwa kuahidi kuishughulikia mara moja kwa kuitengeneza.

Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Dk.Mande amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa sekta binafsi katika kutoa huduma za afya na iko tayari kufanya kazi na kliniki hiyo."Tunawakaribisha muda wowote kufanya kazi katika dhana ya PPP.Kikubwa ambacho tunaweza kueleza hapa ni kwamba tunathamini mchango wenu na tunaomba tuedelee kushirikiana katika kuwahudumia Watanzania,"amesema.

Wakati huo huo mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Kliniki ya Heameda Dk.Reginald Mengi amesema kijana wa Kitanzania Dk.Hery Mwandolela ambaye ndio mmikili wa Kliniki hiyo amefanya maajabu makubwa na anastahili kuwa mfano wa kuigwa.
 Mwenyekiti wa Kampuni za IPP Media Dk.Reginald Mengi (katikati) akiwa pamoja na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Dk.Hery Mwandolela(kulia) na kushoto Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo wakiangalia ujumbe uliopo kwenye jiwe la msingi ikiwa ni ishara ya kuzinduliwa rasmi kwa Kliniki ya Heameda ambayo ni maalum kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu ya magonjwa ya moyo.
 Mkuu wa Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam Daniel Chongolo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Heameda iliyopo Bunju B jijini Dar es Salaam ambapo ameahidi kutatua kero ya barabara inayoelekea kwenye kliniki hiyo
 Mmiliki wa Kliniki ya Heameda ambaye pia ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo Dk.Hery Mwandolela akizungumza wakati wa uzinduzi wa kliniki hiyo leo jijini Dar es Salaam
 Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Kliniki ya Heameda iliyopo Bunju B jijini Dar es Salaam Dk.Reginald Mengi akikabidhi cheti maalum kwa Dk.Isaac Maro kwa kutambua mchango wake  katika kliniki hiyo.



Hivyo makala DC Kinondoni aahidi kutatua kero ya barabara inayokwenda Kliniki ya Heameda, Mengi ashangazwa na maajabu ya Dk.Mwandolela

yaani makala yote DC Kinondoni aahidi kutatua kero ya barabara inayokwenda Kliniki ya Heameda, Mengi ashangazwa na maajabu ya Dk.Mwandolela Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC Kinondoni aahidi kutatua kero ya barabara inayokwenda Kliniki ya Heameda, Mengi ashangazwa na maajabu ya Dk.Mwandolela mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/dc-kinondoni-aahidi-kutatua-kero-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DC Kinondoni aahidi kutatua kero ya barabara inayokwenda Kliniki ya Heameda, Mengi ashangazwa na maajabu ya Dk.Mwandolela"

Post a Comment