title : WANACHAMA 15 KUTOKA VYAMA VYA UPINZANI WAJIUNGA NA CCM
kiungo : WANACHAMA 15 KUTOKA VYAMA VYA UPINZANI WAJIUNGA NA CCM
WANACHAMA 15 KUTOKA VYAMA VYA UPINZANI WAJIUNGA NA CCM
WANACHAMA 15 wa vyama vya siasa vya upinzani wilaya ya Temeke wamejiunga na chama cha Mapinduzi CCM jijini Dar es Salaam leo.
Wanachama waliohama vyama vyao na kujiunga na CCM ni aliyekuwa katibu CHADEMA kata ya chang'ombe Abduli Kheri, Mwenyekiti CHADEMA Kata ya toangoma John Matugura, aliyekuwa katibu CHADEMA kata ya Temeke na katibu na mwenyekiti wa Bavicha wilaya ya TemekeChales Gahu, Afisa uchaguzi CHADEMA katibu mwenezi ACT WazalendoSteven Shekumkae.
Mwanachama CHADEMA Saidi Mohamed Ngaola,Mwenyekiti CHADEMA kata ya Kurasini James Nyaki, Mwanachama CHADEMA Mahamudu Saidani, Katibu mwenezi CHADEMA kata ya MtoniThomas Elia, Mwanachama CHADEMA Juma Said, Mwenyekiti Vijana Chama cha ACT Wazalendo KelvinAbiud ,Wanachama wa ACT Wazalendo Editha Bunjoro (Mama Kelvini,) Taifa baraza la wadhamini CHADEMA,Katibu kata CUF Toangoma Ally Mbonde,Renaty Lipambile Mwenyekiti CHADEMA wilaya ya Temeke na diwani wa kata ya mtoni Bernard Mwakyembe.
Wakizungumza mara baada ya kurudisha kadi za vyama vyao wanachama hao wamesema kuwa hawajanunuliwa bali wanaunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli baada ya kuona utekelezaji wake.
Akizungumza wakati wa kuwapokea katika chama cha Mapinduzi CCM katibu Mwenezi wa chama cha Mapinduzi CCM, Humfrey Polepole jijini Dar es Salaam leo amewakaribisha katika kwenye chama Tawala CCM.
Amesema kuwa utaratibu wa kupata kadi zao za Chama cha mapinduzi watazipata kwenye mashina wanakoishi kama utaratibu ulivyopangwa na Chama cha Mapinduzi.
Pia Polepole amesema kuwa Wanawake wa chama cha mapinduzi watanufaika na mikopo isiyona riba kwani chama kimechoka na mikopo kutoka sehemu nyingine na yenye riba.
Baadhi ya wanachama kutoka vyama vya upinzani wilaya ya Temeke wakiwa mbele mara baada ya kupkelewa katika chama Cha Mapinduzi CCM jijini Dar es Salaam leo.
Mwanachama mpya akifungwa skafu ya CCM.
Wanacham wapya wa CCM wakirudisha kadi zao za vyama walikokuwa.
Hivyo makala WANACHAMA 15 KUTOKA VYAMA VYA UPINZANI WAJIUNGA NA CCM
yaani makala yote WANACHAMA 15 KUTOKA VYAMA VYA UPINZANI WAJIUNGA NA CCM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANACHAMA 15 KUTOKA VYAMA VYA UPINZANI WAJIUNGA NA CCM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/wanachama-15-kutoka-vyama-vya-upinzani.html
0 Response to "WANACHAMA 15 KUTOKA VYAMA VYA UPINZANI WAJIUNGA NA CCM"
Post a Comment