BALOZI WA KENYA AFANYA ZIARA SIMIYU KUJIONEA FURSA ZA UWEKEZAJI

BALOZI WA KENYA AFANYA ZIARA SIMIYU KUJIONEA FURSA ZA UWEKEZAJI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BALOZI WA KENYA AFANYA ZIARA SIMIYU KUJIONEA FURSA ZA UWEKEZAJI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BALOZI WA KENYA AFANYA ZIARA SIMIYU KUJIONEA FURSA ZA UWEKEZAJI
kiungo : BALOZI WA KENYA AFANYA ZIARA SIMIYU KUJIONEA FURSA ZA UWEKEZAJI

soma pia


BALOZI WA KENYA AFANYA ZIARA SIMIYU KUJIONEA FURSA ZA UWEKEZAJI

Na Stella Kalinga, Simiyu

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu amefanya ziara mkoani Simiyu Oktoba 03, 2018 na kuzungumza na viongozi wa mkoa huo, ambapo ameeleza kuwa moja ya malengo ya ziara yake ni kufahamu Mipango na Fursa za Uwekezaji zilizopo mkoani Simiyu, ili aweze kuzungumza na wawekezaji nchini Kenya kuwekeza mkoani humo.

Balozi Kazungu amesema nchi ya Kenya ndiyo inaongoza kuwekeza nchini Tanzania ukilinganishwa na nchi nyingine za Afrika ambapo hadi sasa imewekeza takribani dola za Kimarekani bilioni 1.6 hapa nchini.“ Nimekuja hapa ili tufahamiane vizuri, nijue mipangilio yenu, fursa za uwekezaji ziko wapi ili tuweze kuzungumzana wenzetu wakaja kuwekeza, Kenya ni nchi inayoongoza kwa kuwekeza nchini Tanzania, hadi sasa imewekeza takribani dola bilioni 1.6 ” alisema Balozi Kazungu.

Aidha, ameomba ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya uendelee kuimarishwa kwa lengo la kuzifanya nchi hizi kuwa shina la viwanda na uwekezaji na kuwa wanufaika wa soko la pamoja la Afrika hali itakayochangia kuimarisha uchumi wa nchi hizo.Pamoja na ushirikiano katika masuala ya uwekezaji na viwanda Balozi Kazungu amesisitiza masuala ya ujirani mwema, upendo na ushirikiano wa kindugu baina ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo inakaribisha sekta binafsi na iko tayari kutoa ardhi bure kwa wawekezaji walio tayari kuwekeza Simiyu katika maeneo yanayojibu mahitaji ya mkoa na nchi kupitia malighafi zinazolishwa ndani ya mkoa na ndani ya nchi.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akimkabidhi Nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Simiyu Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu, wakati wa ziara yake mkoani humo, Oktoba 03, 2018.
Kutoka kulia Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini, Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka, Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu na Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuchambua Pamba cha Alliance Ginnery kilichopo Bariadi, Bw. Boaz Ogola wakiteta jambo, wakati wa ziara ya Balozi huyo mkoani Simiyu, Oktoba 03, 2018.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu , Mjini Bariadi wakati wa ziara yake mkoani humo, Oktoba 03, 2018.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu ( wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Simiyu mara baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani Simiyu, Oktoba 03, 2018.



Hivyo makala BALOZI WA KENYA AFANYA ZIARA SIMIYU KUJIONEA FURSA ZA UWEKEZAJI

yaani makala yote BALOZI WA KENYA AFANYA ZIARA SIMIYU KUJIONEA FURSA ZA UWEKEZAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI WA KENYA AFANYA ZIARA SIMIYU KUJIONEA FURSA ZA UWEKEZAJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/balozi-wa-kenya-afanya-ziara-simiyu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BALOZI WA KENYA AFANYA ZIARA SIMIYU KUJIONEA FURSA ZA UWEKEZAJI"

Post a Comment