AFREXIMBANK KUIPATIA TANZANIA ZAIDI YA SH. TRILIONI MOJA KUGHARAMIA UJENZI WA RELI NA VITUO VYA BIASHARA

AFREXIMBANK KUIPATIA TANZANIA ZAIDI YA SH. TRILIONI MOJA KUGHARAMIA UJENZI WA RELI NA VITUO VYA BIASHARA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AFREXIMBANK KUIPATIA TANZANIA ZAIDI YA SH. TRILIONI MOJA KUGHARAMIA UJENZI WA RELI NA VITUO VYA BIASHARA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AFREXIMBANK KUIPATIA TANZANIA ZAIDI YA SH. TRILIONI MOJA KUGHARAMIA UJENZI WA RELI NA VITUO VYA BIASHARA
kiungo : AFREXIMBANK KUIPATIA TANZANIA ZAIDI YA SH. TRILIONI MOJA KUGHARAMIA UJENZI WA RELI NA VITUO VYA BIASHARA

soma pia


AFREXIMBANK KUIPATIA TANZANIA ZAIDI YA SH. TRILIONI MOJA KUGHARAMIA UJENZI WA RELI NA VITUO VYA BIASHARA

Na: WFM,  Mjini Bali Indonesia
African Export Import Bank (Afreximbank) ya Misri, imeonyesha nia ya kuipatia Tanzania mkopo wa zaidi ya Shilingi trilioni moja (dola za Marekani zaidi ya milioni 500) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kipaumbele hasa ya miundombinu ya reli na kujenga vituo vya biashara (SEZ and Industrial parks).
Hayo yalibainishwa mjini Bali Indonesia, na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango baada ya Mkutano na Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel,  uliofanyika  wakati wa mikutano ya mwaka  ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ikiendelea.
Waziri Mpango, alisema kuwa Afreximbank imethibitisha kuwa ipo tayari kutoa mkopo wa  dola za Marekani milioni 125  (takribani Shilingi bilioni 285.9) kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Kimataifa  (SGR),  kipande cha Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma.
“Afreximbank wanania pia ya kutoa  dola milioni 400 (takribani Sh. Bilioni 914.9) ambazo wanaweza kutukopesha kwa ajili ya kugharamia miradi ya miundombinu itakayorahisisha biashara kati ya Tanzania na nchi jirani na Bara la Afrika kwa ujumla,  ili kuchochea kasi ya ukuaji wa biashara katika nchi hizo kwa lengo la kuondoa umasikini”, aliongeza Dkt. Mpango.
Alisema kuwa kwa kuwa tayari Tanzania ilikuwa na mkakati wa kufungua vituo vya biashara katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na mikoa mingine, suala la mkopo huo ni fursa kubwa kwa  maendeleo ya nchi, hivyo jambo hilo litafanyiwa kazi kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji  na Sekta Binafsi, ili Taifa liweze kunufaika na fedha ambazo benki hiyo ipo tayari kuzitoa.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akizungumzia miradi ya miundombinu ikiwemo ya Reli ya Kisasa kwa kiwango cha kimataifa, katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi, wakati wa Mkutano na Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel, uliofanyika Bali Indonesia, kulia ni Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga.
Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga, na Afisa Mwandamizi wa Wizara hiyo Bw. Elias Shosi, wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel, alipokuwa akizungumzia maamuzi ya benki yake kuikopesha Tanzania zaidi ya Shilingi trilioni moja wakati wa mkutano uliofanyika Bali, Indonesia.
Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga, na Afisa Mwandamizi wa Wizara hiyo Bw. Elias Shosi, wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel, alipokuwa akizungumzia maamuzi ya benki yake kuikopesha Tanzania zaidi ya Shilingi trilioni moja wakati wa mkutano uliofanyika Bali, Indonesia.
Meneja wa Afreximbank Kanda ya Afrika Mashariki Bw. Kudakwashe Matereke, akieleza jambo wakati wa Mkutano kati ya Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hawapo pichani), mjini Bali Indonesia wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel, wakipeana mkono baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao uliofanyika mjini Bali Indonesia wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)



Hivyo makala AFREXIMBANK KUIPATIA TANZANIA ZAIDI YA SH. TRILIONI MOJA KUGHARAMIA UJENZI WA RELI NA VITUO VYA BIASHARA

yaani makala yote AFREXIMBANK KUIPATIA TANZANIA ZAIDI YA SH. TRILIONI MOJA KUGHARAMIA UJENZI WA RELI NA VITUO VYA BIASHARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AFREXIMBANK KUIPATIA TANZANIA ZAIDI YA SH. TRILIONI MOJA KUGHARAMIA UJENZI WA RELI NA VITUO VYA BIASHARA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/afreximbank-kuipatia-tanzania-zaidi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "AFREXIMBANK KUIPATIA TANZANIA ZAIDI YA SH. TRILIONI MOJA KUGHARAMIA UJENZI WA RELI NA VITUO VYA BIASHARA"

Post a Comment