title : KATIBU TAWALA KIGAMBONI AGAWA HUNDI ZA MIKOPO YA AKINA MAMA,SOMA HAPA YAJAYO YANAFURAHISHA.
kiungo : KATIBU TAWALA KIGAMBONI AGAWA HUNDI ZA MIKOPO YA AKINA MAMA,SOMA HAPA YAJAYO YANAFURAHISHA.
KATIBU TAWALA KIGAMBONI AGAWA HUNDI ZA MIKOPO YA AKINA MAMA,SOMA HAPA YAJAYO YANAFURAHISHA.
Na .John Luhende
Mwamba wa habari
Halmashauri ya manispaa ya Kigambo leo imeanza kutoa Mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya akina mama, ambapo vikundi 23 vilivyo kidhi vigezo vimepatiwa mkopo wenye thamani ya shilingi million 45 bila riba.
Akizungumza kataika hafla ya kugawa hundi kwa vikundi hivyo vya akinamama Katibu tawala wa Wilaya ya Kigamboni Raheli Mhando amevitaka vikundihivo kuzitumiafedha hizo katika kuendeleza biashara zao na kuzingatia muda wa kurejesha ili ili waweze kuongezewa zaidi.
‘’Wilaya yetu bado ni changa tutaendelea kuongeza fedha zaidi kadiri ya uwezo wa Manispaa yetu, naomba mjitahidi kurejesha kwa wakati na mkikwama msikae kimya mje kutoa taarifa hatuwezi kuajakuuza vitu vyenu tutawaelewa tunaweza kuwaongezea muda Serikali yenu sikivu ina wajali‘’alisema
Aidha Mhando amesema pamoja na kuanza kutoa mikopo hiyo kwa akina mama,halmashauri inatoa mikopo kwa vijana na walevu ambapo inaendelea kufanyiakazi taarifa za vikundi 18 vyavijana ambavyo vina tarajiwa kukopeshwa Pikipiki.
’’Waambieni huko na ndugu zetu walemavu waje kuchukua mikopo kwasasa idara inaendelea kufanyia kazi maelekezo ya mkuu wa Wilaya kwamba mikopo ya pikipiki itolewe kwa vikundi na siyo kwa mtu mmoja ikikamilika vija nao watapewa Pikipiki “ alisema
Naye Afisa Maendeleo wa Manispaa ya Kigamboni Said Bakari , amesema Fedha hizo zitaendelea kutolewa kama serikali ilivyo agiza ,ambapo agizo la Serikali ni kutoa asilimia kumi ya mapato kwa mgawanyo wa asilimia 4% vijana asilimia 4 %vijana na asilimia 2% kwa walemavu na sasa ni sheria na wataendelea kuitekeleza.
Kwaupande wao wanawake walipewa hudi hizo wameishukuru serikali ya awamu yatano kwa utaratibumzuri wa kuwakopesha lakini wameomba kiasi cha mkopo huo kiweze kuongezwa pindi wanapo kamilisha marejesho.
‘’Tuna shukuru kwa mikopo hii itatusaidia sana sisi akinamama na biashara zetu tutajitahidi kurejesha kwa wakati ili tupewe zaidi na ninawaomba akimama wenzangu tujitahidi kurejesha .
“Alisema Sophia Mario mwenyekiti wa kikundi cha Milango saba Vikoba Group.
Hivyo makala KATIBU TAWALA KIGAMBONI AGAWA HUNDI ZA MIKOPO YA AKINA MAMA,SOMA HAPA YAJAYO YANAFURAHISHA.
yaani makala yote KATIBU TAWALA KIGAMBONI AGAWA HUNDI ZA MIKOPO YA AKINA MAMA,SOMA HAPA YAJAYO YANAFURAHISHA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU TAWALA KIGAMBONI AGAWA HUNDI ZA MIKOPO YA AKINA MAMA,SOMA HAPA YAJAYO YANAFURAHISHA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/katibu-tawala-kigamboni-agawa-hundi-za.html
0 Response to "KATIBU TAWALA KIGAMBONI AGAWA HUNDI ZA MIKOPO YA AKINA MAMA,SOMA HAPA YAJAYO YANAFURAHISHA."
Post a Comment