title : WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU WATUMISHI WIZARA YAKE KUNYANYASWA, AFUNGUA MILANGO KULETA KERO ZAO OFISINI KWAKE
kiungo : WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU WATUMISHI WIZARA YAKE KUNYANYASWA, AFUNGUA MILANGO KULETA KERO ZAO OFISINI KWAKE
WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU WATUMISHI WIZARA YAKE KUNYANYASWA, AFUNGUA MILANGO KULETA KERO ZAO OFISINI KWAKE
Na Felix Mwagara, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka viongozi na watumishi mbalimbali wa wizara yake wafanye kazi kwa kushirikiana na kuacha tabia ya kunyanyasana wakati wanatekeleza majukumu yao ya kikazi.
Lugola pia amesema kila mtumishi wa wizara yake ana umuhimu mkubwa kwa kufanikisha mafanikio ya wizara hiyo kwakuwa watumishi hao wanafanya kazi kwa kutegemeana. Akizungumza na watumishi wa makao makuu wa wizara hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Veta, jijini Dodoma jana, Lugola alisema kikao hicho alikiitisha kwa lengo la kujuana na watumishi hao pamoja na kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi.
“Mambo muhimu ambayo yatatuletea mafanikio ndani ya wizara yetu ni kufanya kazi kwa bidii, kufanya kazi kwa kushirikiana na tukifanya hivyo hakika tutapendana na kuzidi kufanikiwa,” alisema Lugola.
Lugola aliongeza kuwa, hapendi kuona mtumishi yeyote ananyanyaswa kwa kutopewa haki zake au kucheleweshewa pasipo kuwa na sababu za msingi ikiwemo malipo mbalimbali ya watumishi wanayodai, na endapo yatatokea hayo watumishi hao wamletee kero zinazowakabili ofisini kwake na kwa kushirikiana na katibu mkuu wa wizara hiyo watazitatua.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na watumishi wa Wizara yake, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi. Pia Lugola aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na kuwataka baadhi ya viongozi wa wizara hiyo kuacha tabia ya kuwanyanyasa watumishi wao. Lugola alikutana na watumishi hao katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Veta, jijini Dodoma, leo jana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu alipokua anawasili katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Veta, jijini Dodoma kwa ajili ya kuzungumza na watumishi wa wizara hiyo, leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhan Kailima. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU WATUMISHI WIZARA YAKE KUNYANYASWA, AFUNGUA MILANGO KULETA KERO ZAO OFISINI KWAKE
yaani makala yote WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU WATUMISHI WIZARA YAKE KUNYANYASWA, AFUNGUA MILANGO KULETA KERO ZAO OFISINI KWAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU WATUMISHI WIZARA YAKE KUNYANYASWA, AFUNGUA MILANGO KULETA KERO ZAO OFISINI KWAKE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/waziri-lugola-apiga-marufuku-watumishi.html
0 Response to "WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU WATUMISHI WIZARA YAKE KUNYANYASWA, AFUNGUA MILANGO KULETA KERO ZAO OFISINI KWAKE"
Post a Comment