Makatibu Wakuu, MaRas Watakiwa Kuzingatia Taratibu, Kanuni na Sheria kwa Maendeleo Wananchi.

Makatibu Wakuu, MaRas Watakiwa Kuzingatia Taratibu, Kanuni na Sheria kwa Maendeleo Wananchi. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Makatibu Wakuu, MaRas Watakiwa Kuzingatia Taratibu, Kanuni na Sheria kwa Maendeleo Wananchi., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Makatibu Wakuu, MaRas Watakiwa Kuzingatia Taratibu, Kanuni na Sheria kwa Maendeleo Wananchi.
kiungo : Makatibu Wakuu, MaRas Watakiwa Kuzingatia Taratibu, Kanuni na Sheria kwa Maendeleo Wananchi.

soma pia


Makatibu Wakuu, MaRas Watakiwa Kuzingatia Taratibu, Kanuni na Sheria kwa Maendeleo Wananchi.

Na Frank Mvungi- MAELEZO
Katibu  Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi amewataka Makatibu Wakuu wa Wizara na Makatibu Tawala wa Mikoa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria , Kanuni, Taratibu na Miongozo inayotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano  kila wanapofanya maamuzi.
Akizungumza leo Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha siku tatu kwa Viongozi hao Balozi Kijazi amesema kuwa  wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanazingatia taratibu zote ili azma ya kujenga uchumi wa viwanda ifikiwe kwa wakati na kuwanufaisha wananchi.
“Nafasi zenu ni za maamuzi hivyo msipofanya maamuzi sahihi na kwa wakati mtakwamisha shughuli za maendeleo na huduma muhimu kwa wananchi.” Alisisitiza Mhandisi Kijazi.
Akifafanua, Mhandisi Kijazi amesema kuwa wajumbe wa mkutano huo wanalojukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanafanyia kazi masuala yote yatakayoazimiwa katika kikao kazi hicho cha siku tatu kinacholenga kuongeza tija katika ngazi ya Wizara na Mikoa kwa kuzingatia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano yakuleta mageuzi makubwa katika nyanza zote hasa katika huduma zinazotolewa kwa wananchi.
Aliongeza kuwa Kikao kazi hicho kina umuhimu mkubwa na kitakuwa kikifanyika kila mwaka ili kuwapa fursa Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala  kubadilishana uzoefu, kubaini changamoto zilizopo na kuweka utaratibu mzuri wa kuzitatua kwa maslahi ya wanachi.
  Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi akifungua  Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
 Mtendaji Mkuuwa Taasisi ya Uongozi Prof.   Joseph  Semboja akisistiza jambo wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
 Sehemu ya Makatibu Wakuu wakifuatilia uwasilisjhaji wa mada mbalimbali  kwenye Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini  Bw.  James Syanga akiwasilisha mada kuhusu athari za madawa ya kulevya wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
  Manaibu Katibu Wakuu  na  Makatibu Tawala wakifuatilia mada wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
Sehemu ya washiriki wa Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu wa Wizara na Makatibu Tawala wa Mikoa wakifuatilia kikao kazi chao kinachoendelea Jijijini Dodoma. (Picha zote na Frank  Shija- MAELEZO)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Makatibu Wakuu, MaRas Watakiwa Kuzingatia Taratibu, Kanuni na Sheria kwa Maendeleo Wananchi.

yaani makala yote Makatibu Wakuu, MaRas Watakiwa Kuzingatia Taratibu, Kanuni na Sheria kwa Maendeleo Wananchi. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Makatibu Wakuu, MaRas Watakiwa Kuzingatia Taratibu, Kanuni na Sheria kwa Maendeleo Wananchi. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/makatibu-wakuu-maras-watakiwa_19.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Makatibu Wakuu, MaRas Watakiwa Kuzingatia Taratibu, Kanuni na Sheria kwa Maendeleo Wananchi."

Post a Comment