title : MAHAKAMA KISUTU KUANZA KUSIKILIZA KESI INAYOMKABILI MENEJA BENKI YA BACLAYS
kiungo : MAHAKAMA KISUTU KUANZA KUSIKILIZA KESI INAYOMKABILI MENEJA BENKI YA BACLAYS
MAHAKAMA KISUTU KUANZA KUSIKILIZA KESI INAYOMKABILI MENEJA BENKI YA BACLAYS
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga kuanza kusikiliza kesi ya wizi wa zaidi ya milioni 390,2 na USD 55,000 na Euro 2,150 inayomkabili aliyekuwa Meneja wa Benki ya Baclays, Alune Kasililika na wenzake 11 kwa siku tatu mfululizo.
Kesi hiyo itaanza kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka kuanzia Oktoba 3,4 na 5 mwaka huu.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya upande wa mashtaka leo Septemba 19 mwaka 2018 kukamilisha upelelezi na washtakiwa hao kusomewa Maelezo ya awali (PH).
Akiwasomea PH , Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono alidai kuwa aliyekuwa Meneja wa Benki ya Barclays Tawi la Kinondoni, Alune Kasilika, aliwasiliana na watuhumiwa wa tukio la ujambazi katika benki hiyo wakiandaa utekelezaji wake.
Kombakono alidai kuwa Aprili 15, mwaka 2014 asubuhi, mshtakiwa Alune Kasililika na Neema Batchu ambao ni wafanyakazi wa benki hiyo, walifika kazini na shughuli za kibenki ziliendelea pamoja na wafanyakazi wengine.
Amedai kuwa Alune, siku hiyo ya tukio alikuwa na mawasiliano na mshtakiwa wa tatu hadi wa tisa ili kuandaa tukio la wizi wa fedha za benki hiyo na hatimaye lilifanyika.
Amedai wizi ulifanikiwa baada ya washtakiwa hao ambao ni wafanyakazi wa benki hiyo kutoa taarifa za kina kuhusu benki kwa mshtakiwa wa tatu hadi wa tisa.
Akiendelea kusoma PH, Wakili Kombakono amedai askari E 9660 D/SSGT Iddy, P407 D/CPL Bundala na Sezary Massawe wakati upelelezi wa kina ukifanyika huku wakijua mshtakiwa wa kwanza hadi wa tisa wanatafutwa kwa wizi, waliwapa taarifa za kiupelelezi ili kuwasaidia wajifiche wasikamatwe na walikimbia kukwepa mkono wa sheria.
Pia mshtakiwa Ruth Macha yeye anadaiwa kuwa alimsaidia mshtakiwa Maulid Seif kutoroka ili kukwepa mkono wa sheria.
Baada ya kumaliza kusomewa PH hizo, Hakimu Shaidi alimtaka kila mshtakiwa kujibu anayokubali na anayokataa ambapo washtakiwa wote walikubali maelezo yao binafsi ikiwamo majina na walikana maelezo yote yanayohusu wizi huo.
Katika kesi hiyo, mshtakiwa wa kwanza hadi wa tisa, wanashtakiwa kwa kula njama kutenda kosa la wizi wa fedha za Benki ya Barclays.
Inadaiwa Aprili 15 mwaka 2014 kwa unyang’anyi wa kutumia silaha, washtakiwa hao waliiba Sh. 390,220,000, Dola za Marekani 55,000 na Euro 2,150 mali ya benki hiyo.
Katika shtaka linalowahusu maofisa wa polisi, Iddy na Bundara, wao wanadaiwa kuwasaidia washtakiwa kutoroka ili wasikamatwe na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria. Ambapo walikana mashtaka yote.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni mameneja wawili wa benki hiyo, Alune Kasilika (28), Neema Batchu (26), mfanyabiashara Hamis Shabani au Carlos (34), mkazi wa Magomeni na dereva Manase Genyeka au Mjeshi (35), mkazi wa Tabata.
Wengine ni wafanyabiashara Kakamie Julius (32), Iddy Khamis (32), Sezary Massawe (31), Boniphace Muumba (29), Ruth Macha (30) na maofisa wawili wa polisi, Iddy (33) na Bundala (37). Washtakiwa hao wanatetewa na wakili Nehemiah Nkoko.
Hivyo makala MAHAKAMA KISUTU KUANZA KUSIKILIZA KESI INAYOMKABILI MENEJA BENKI YA BACLAYS
yaani makala yote MAHAKAMA KISUTU KUANZA KUSIKILIZA KESI INAYOMKABILI MENEJA BENKI YA BACLAYS Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA KISUTU KUANZA KUSIKILIZA KESI INAYOMKABILI MENEJA BENKI YA BACLAYS mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/mahakama-kisutu-kuanza-kusikiliza-kesi.html
0 Response to "MAHAKAMA KISUTU KUANZA KUSIKILIZA KESI INAYOMKABILI MENEJA BENKI YA BACLAYS"
Post a Comment