SERIKALI KUENDELEA KUELIMISHA JAMII NA WADAU KUHUSU URIDHIAJI WA MIKATABA.

SERIKALI KUENDELEA KUELIMISHA JAMII NA WADAU KUHUSU URIDHIAJI WA MIKATABA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI KUENDELEA KUELIMISHA JAMII NA WADAU KUHUSU URIDHIAJI WA MIKATABA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI KUENDELEA KUELIMISHA JAMII NA WADAU KUHUSU URIDHIAJI WA MIKATABA.
kiungo : SERIKALI KUENDELEA KUELIMISHA JAMII NA WADAU KUHUSU URIDHIAJI WA MIKATABA.

soma pia


SERIKALI KUENDELEA KUELIMISHA JAMII NA WADAU KUHUSU URIDHIAJI WA MIKATABA.

Na Daudi Manongi, MAELEZO, DODOMA.

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu  imesema kuwa itaendelea kuelimisha jamii na wadau mbalimbali kuhusu mifumo,maudhui na taratibu za uridhiaji wa mikataba ili kufanya maandalizi stahiki kabla ya uridhiaji wa mikataba hiyo.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi ,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde wakati akijibu Swali la Mhe.Ussi Pondeza Mbunge wa Chambani.
“Nchi yetu inazo sheria mbalimbali zinazotambua na kusimamia maslahi ya wafanyakazi nchini wakiwemo wafanyakazi wa majumbani,wafanyakazi wa mahotelini na vyama vyao”,Aliongeza Mhe,Mavunde.

Aidha Waziri Mavunde amewataka wafanyakazi nchini kutambua juhudi za Serikali za kulinda na kutetea haki na maslahi  ya wafanyakazi kupitia sheria,kanuni na taratibu zilizopo nchini.

Amesema Serikali inaendelea kupitia kwa makini azimio lililofikiwa na Shirika la kazi la Umoja wa Mataifa mwaka 2011 linaotaka kila nchi mwanachama wa ILO kuwa na Sheria ya kuwalinda wafanyakazi wa Mahotelini na Majumbani.

“Ni kweli kuwa Mwaka 2011,Nchi wanachama wa Shirika la Kazi Duniani ikiwemo Tanzania zilipitisha mkataba wa kimataifa kuhusu kazi za Staha kwa wafanyakazi wa Majumbani,ambapo hadi sasa nchi zilizoridhia ni 23 kati ya nchi 189 na kwa upande wa Afrika zimelizia nchi mbili tu kwa iyo bado tunaendelea kuupitia ili kufanya maandalizi ya kuridhia”,Aliongeza Mhe.Mavunde.

Pamoja na hayo Waziri Mavunde amesisitiza kuwa Tanzania Bara ina sheria zake za kazi ambazo zinawahusu wafanyakazi wote  ikiwemo wafanyakazi wa mahotelini na majumbani ambazo zinalinda haki zao.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi ,Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 22, 2017. 


Hivyo makala SERIKALI KUENDELEA KUELIMISHA JAMII NA WADAU KUHUSU URIDHIAJI WA MIKATABA.

yaani makala yote SERIKALI KUENDELEA KUELIMISHA JAMII NA WADAU KUHUSU URIDHIAJI WA MIKATABA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUENDELEA KUELIMISHA JAMII NA WADAU KUHUSU URIDHIAJI WA MIKATABA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/serikali-kuendelea-kuelimisha-jamii-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI KUENDELEA KUELIMISHA JAMII NA WADAU KUHUSU URIDHIAJI WA MIKATABA."

Post a Comment