WABUNGE WANAWAKE WAKUSANYA BIL 2.5/-KUJENGA CHOO CHA MFANO KWA MAJIMBO YOTE NCHINI

WABUNGE WANAWAKE WAKUSANYA BIL 2.5/-KUJENGA CHOO CHA MFANO KWA MAJIMBO YOTE NCHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WABUNGE WANAWAKE WAKUSANYA BIL 2.5/-KUJENGA CHOO CHA MFANO KWA MAJIMBO YOTE NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WABUNGE WANAWAKE WAKUSANYA BIL 2.5/-KUJENGA CHOO CHA MFANO KWA MAJIMBO YOTE NCHINI
kiungo : WABUNGE WANAWAKE WAKUSANYA BIL 2.5/-KUJENGA CHOO CHA MFANO KWA MAJIMBO YOTE NCHINI

soma pia


WABUNGE WANAWAKE WAKUSANYA BIL 2.5/-KUJENGA CHOO CHA MFANO KWA MAJIMBO YOTE NCHINI


 Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akipokea hundi kutoka kwa wawakilishi wa benki ya CRDB wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akizungumza wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akipokea hundi kutoka kwa wawakilishi wa makampuni mbalimbali wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akipokea hundi kutoka kwa wawakilishi wa benki ya NBC wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

*Spika mstaafu Makinda ashangazwa… atoa neno 
*Dk.Tulia asema ili kufanikisha lengo zinahitaji Bil 3.5/- 
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

CHAMA cha Wabunge Wanawake wa Bunge la Tanzania wamefanikiwa kukusanya Sh.milioni 800 kwenye harambee ya kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa choo kitakachojengwa katika majimbo yote nchini.

Fedha hizo zimekusanywa jana kwenye harambee iliyofanyika Mliman City jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi kwenye harambee hiyo alikuwa Spika wa Bunge mstaafu Anne Makinda.

Tayari wabunge hao wanawake wamefanikiwa kukusanya jumla ya Sh.bilioni 2.5 kwani kabla ya harambee ya jana tayari walishafanya harambee nyingine ya kukusanya fedha jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa harambee hiyo Spika wa Bunge Job Ndugai amesema wanatambua umuhimu wa kuunga mkono jitihada za wabunge wanawake katika kuhakikisha wanatimiza lengo la ujenzi wa choo.

“Tumekutana hapa kwa lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyoo.Lengo ni kujenga vyoo nchi nzima kwa maana ya majimbo yote,”amesema Ndugai.

Kwa upande wa mgeni rasmi Spika mstaafu wa Bunge Makinda amesema uamuzi ambao umefanywa na wabunge wanawake na kuungwa mkono na wabunge wanaume katika kufanikisha fedha zinapatikana ni wa kihistoria.

“Tunatambua changamoto ambazo wanafunzi wanazipata na hasa kwa mtoto wa kike kutokana na maumbile yake.Hivyo ujenzi wa choo cha mfano kitasaidia kuwafanya wanafunzi hao kufurahia mazingira yatakayokuwamo kwenye choo hicho.

“Tunafahamu binti wa kike anapovunja ungo akiwa shuleni kuna mabadiliko yanaanza kutokea na anapokuwa kwenye tarehe yake wengine wanatega shuleni kwa kuona hawako salama.Choo kitakachojengwa kitamfanya binti kutokuwa na wasiwasi hata akiwa kwenye tarehe za hedhi,”amefafanua.
Makinda ametoa ombi kwa Watanzania kokote walipo kuchangia ujenzi wa choo hicho kwani lengo na kumuondolea adha mwanafunzi na hasa mwanafunzi wa kike.


Hivyo makala WABUNGE WANAWAKE WAKUSANYA BIL 2.5/-KUJENGA CHOO CHA MFANO KWA MAJIMBO YOTE NCHINI

yaani makala yote WABUNGE WANAWAKE WAKUSANYA BIL 2.5/-KUJENGA CHOO CHA MFANO KWA MAJIMBO YOTE NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WABUNGE WANAWAKE WAKUSANYA BIL 2.5/-KUJENGA CHOO CHA MFANO KWA MAJIMBO YOTE NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/wabunge-wanawake-wakusanya-bil-25.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WABUNGE WANAWAKE WAKUSANYA BIL 2.5/-KUJENGA CHOO CHA MFANO KWA MAJIMBO YOTE NCHINI"

Post a Comment