JAMII IMEHIMIZWA KUZINGATIA UZAZI WA MPANGO

JAMII IMEHIMIZWA KUZINGATIA UZAZI WA MPANGO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JAMII IMEHIMIZWA KUZINGATIA UZAZI WA MPANGO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JAMII IMEHIMIZWA KUZINGATIA UZAZI WA MPANGO
kiungo : JAMII IMEHIMIZWA KUZINGATIA UZAZI WA MPANGO

soma pia


JAMII IMEHIMIZWA KUZINGATIA UZAZI WA MPANGO






Na: Veronica Kazimoto


JAMII imehimizwa kuzingatia uzazi wa mpango ili kupata familia bora ambazo watamudu kuzihudumia katika mahitaji muhimu ambayo ni elimu, chakula na malazi.


Hayo yamesemwa  na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Otilia Gowele wakati wa maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Duniani iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mwembe Yanga.

Dkt. Gowele amesema ni muhimu kwa jamii kutumia njia za uzazi wa mpango ili kupanga familia waitakayo na yenye tija katika kuihudumia kwenye mahitaji muhimu.

“Leo tunaadhimisha Siku ya Idadi ya Watu Duniani yenye kauli mbiu isemayo ‘Uzazi wa Mpango; Huwezesha watu; Huendeleza Mataifa’. Hii inatukumbusha kwamba, kila mmoja wetu anatakiwa kutumia njia za uzazi wa mpango ili kupata familia iliyo bora ambayo anaweza kuimudu.
 
Tukiwa na familia ambazo zinazingatia uzazi wa mpango, tutapunguza vifo vya akina mama wajawazito, tutasaidia watoto kukua wakiwa na afya njema kwa kupata mahitaji yao muhimu pamoja na kuiwezesha Serikali kuwahudumia wananchi wake,” amesema Dkt. Gowele

Amesema Wizara ya Afya itaendelea kuhimiza wananchi kutumia uzazi wa mpango ili kufanikisha azma ya Serikali katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na wananchi wenye afya bora.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shughuli za Kitwakimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya amesema kwa mujibu wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania wa Mwaka 2015/16, amesema takribani wanawake 4 kati ya 10 walioolewa ambao ni sawa na asilimia 38 wanatumia njia yeyote ya uzazi wa mpango.

Amesema asilimia 32 ya wanawake hao wanatumia njia za kisasa na asilimia 6 wanatumia njia za asili. Njia ya kisasa inayotumika zaidi ni sindano kwa asilimia 13 ikifuatiwa na vipandikizi kwa asilimia 7 na vidonge kwa asilimia 6.

Irenius Ruyobya amesema kuwa NBS itaendelea  kutoa takwimu rasmi zinazohusiana na masuala ya afya kwa kushirikiana na Wizara ya Afya pamoja na wadau wengine ili kuiwezesha Serikali kupanga mipango mbalimbali ya kuwahudumia wananchi wake.

Maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Duniani huazimishwa kila mwaka tarehe 11 Julai ambapo mratibu mkuu ni Tume ya Mipango chini ya Wizara ya Fedha na Mipango ikishirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulika na Idadi ya Watu Duniani (UNFPA)


Hivyo makala JAMII IMEHIMIZWA KUZINGATIA UZAZI WA MPANGO

yaani makala yote JAMII IMEHIMIZWA KUZINGATIA UZAZI WA MPANGO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JAMII IMEHIMIZWA KUZINGATIA UZAZI WA MPANGO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/jamii-imehimizwa-kuzingatia-uzazi-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "JAMII IMEHIMIZWA KUZINGATIA UZAZI WA MPANGO"

Post a Comment