title : UMOJA WA VILABU VYA WAANDISHI WA HABARI WAMPA TUZO AZORY GWANDA
kiungo : UMOJA WA VILABU VYA WAANDISHI WA HABARI WAMPA TUZO AZORY GWANDA
UMOJA WA VILABU VYA WAANDISHI WA HABARI WAMPA TUZO AZORY GWANDA
Absolom Kibanda.
Na Seif Mangwangi,Arusha
UMOJA wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC), imemtangaza Mwandishi Azory Gwanda ambaye amepotea katika mazingira ya kutatanisha Novemba mwaka jana kuwa mshindi wa tuzo ya Daudi Mwangosi kwa mwaka 2018.
Gwanda aliyekuwa mfanyakazi wa kampuni ya mwananchi communication akiandikia gazeti la Mwananchi alipotea katika mazingira ya kutatanisha akiwa katika kazi zake za kihabari katika maeneo ya Kibiti na Rufiji.
Tuzo hiyo ya Daudi Mwangosi sambamba na kiasi cha shilingi milioni kumi (10), alikabidhiwa mke wa Gwanda, katika mkutano mkuu wa mwaka wa UTPC.
Mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo hiyo, Absolom Kibanda aliiomba Serikali kutofumbia macho matukio ya utekaji wa waandishi wa habari kwa kuwa yanatoa ishara mbaya kwa jamii na kuminya uhuru wa habari.
Alisema Rais Dkt John Magufuli amekuwa rafiki mkubwa wa vyombo vya habari hivyo alimtaka kutoishia kuwa rafiki na badala yake achukue hatua dhidi ya matukio ya utekwaji na kuteswa kwa waandishi wa habari.
Hivyo makala UMOJA WA VILABU VYA WAANDISHI WA HABARI WAMPA TUZO AZORY GWANDA
yaani makala yote UMOJA WA VILABU VYA WAANDISHI WA HABARI WAMPA TUZO AZORY GWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UMOJA WA VILABU VYA WAANDISHI WA HABARI WAMPA TUZO AZORY GWANDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/umoja-wa-vilabu-vya-waandishi-wa-habari.html
0 Response to "UMOJA WA VILABU VYA WAANDISHI WA HABARI WAMPA TUZO AZORY GWANDA"
Post a Comment