WAZIRI MKUU MAJALIWA APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA KUCHUNGUZA AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE

WAZIRI MKUU MAJALIWA APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA KUCHUNGUZA AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU MAJALIWA APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA KUCHUNGUZA AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU MAJALIWA APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA KUCHUNGUZA AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE
kiungo : WAZIRI MKUU MAJALIWA APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA KUCHUNGUZA AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE

soma pia


WAZIRI MKUU MAJALIWA APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA KUCHUNGUZA AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea ripoti ya uchunguzi wa  ajali ya kivuko cha MV Nyerere kutoka kwa kamati iliyoundwa na Serikali kwa ajili ya kuchunguza ajali hiyo.

Amepokea ripoti hiyo leo (Alhamisi, Oktoba 25, 2018) kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati  hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstafu, Jenerali George Waitara,kwenye makazi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuishikuru kamati hiyo kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi kubwa waliyoifanya ambayo imethibitisha umakini wao.

Pia ameipongeza kamati hiyo kwa namna walivyotumia muda wao vizuri kwa kufanya kazi hiyo na kutoa mapendekezo kwa Serikali juu ya mambo waliyoyabaini.

“Nimepokea taarifa kwa niaba ya Serikali, Serikali itafanya mapitio ya taarifa yote na viambatisho vyake na itapitia kwa kina mapendekezo mliyoyatoa ambayo yote yatafanyiwa kazi.”

Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali inaamini mambo yote yaliyosheheni katika taarifa hiyo ni yale ambayo Watanzania wanasubiri kuona yakifanyiwa kazi.

MV Nyerere ilipindika na kuzama Septemba 20, mwaka huu katika ziwa Victoria ambapo Watanzania zaidi 200 walipoteza maisha na wengine Zaidi ya 40 waliokolewa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Ripoti ya Kamati iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati  hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstafu, Jenerali George Waitara, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha  Ripoti ya Kamati iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere  baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali George Waitara (kushoto) kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018.  
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere baada ya kupokea Ripoti ya Kamati hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera na Uratibu, Profesa Faustin Kamuzora na  wapili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali George Waitara.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati  iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere  baada ya kupokea Ripoti ya Kamati hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera  na Uratibu) Profesa Faustin Kamuzora na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali George Waitara.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na Mwenyekiti wa Kamati  iliyoundwa na Serikali  Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali, George Waitara  baada ya kupokea Ripoti ya Kamati hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala WAZIRI MKUU MAJALIWA APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA KUCHUNGUZA AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE

yaani makala yote WAZIRI MKUU MAJALIWA APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA KUCHUNGUZA AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU MAJALIWA APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA KUCHUNGUZA AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/waziri-mkuu-majaliwa-apokea-ripoti-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUU MAJALIWA APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA KUCHUNGUZA AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE"

Post a Comment