DC PANGANI AWATAKA WASHIRIKI WA MISS TANZANIA KUTANGAZA UTALII

DC PANGANI AWATAKA WASHIRIKI WA MISS TANZANIA KUTANGAZA UTALII - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC PANGANI AWATAKA WASHIRIKI WA MISS TANZANIA KUTANGAZA UTALII, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC PANGANI AWATAKA WASHIRIKI WA MISS TANZANIA KUTANGAZA UTALII
kiungo : DC PANGANI AWATAKA WASHIRIKI WA MISS TANZANIA KUTANGAZA UTALII

soma pia


DC PANGANI AWATAKA WASHIRIKI WA MISS TANZANIA KUTANGAZA UTALII

Washiriki wa Miss Tanzania 2018.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Pangani Zainab Abdallah amewataka washiriki wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania mwaka 2018 kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Amesema lengo ni  kusaidia kuongeza idadi ya watalii nchini huku akiwahakikishia warembo hao Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli imeamua kutoa kipaumbele kwa vijana kutimiza ndoto zao.

Abdallah  ambaye ndio Mkuu wa Wilaya mwenye umri mdogo kwa wakuu wa wilaya nchini amesema hayo wilayani Muheza mkoani Tanga  baada ya kuwapokea warembo 20 wanaoshiriki shindano hilo.

Ambapo walifika mkoani Tanga kwa ajili ya kutembelea vituo vya utalii vinavyosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu nchini(TFS) ambapo amewahakikishia kwenye hifadhi hiyo kuna utalii ambao haupo mahali kokote duniani zaidi ya Misitu ya Amani.

Hivyo amesema ujio wa warembo huo ni muhimu na kuwataka wawe mabalozi wazuri wa kuutangaza utalii

"Tanzania  ina vivutio vingi sana,mfano kwa  wilaya ya Pangani tuna mbuga  Sadan ambayo ndio mbuga ambayo imepakana na bahari barani Afrika.

" Pia tuna majengo ya kale kwa kifupi Pangani haitofautiani na Zanzibar.Tujitahidi kuutangaza utalii wa ndani ili tusaidie kuleta pato la Taifa,"amefafanua.

Ameongeza kupitia utalii wa ndani warembo hao watajipambanua kwakutumka fursa zilizopo ili kujipatia fursa za ajira.

Wakati huo huo Meneja Masoko na Uwekezaji wa TFS Mariam Kobelo  ameeleza kwamba malengo ya kuwapeleka  warembo hao katika vivutio hivyo ili waone vivutio na kisha kuvitangaza vivutio.

"TFS itatumia warembo hao kama chombo cha kutangaza utalii wandani kwa upande wa mazingira,kwa kufanya hivyo watasaidia kuongeza pato kwa sbabu tutawatumia kama chombo cha kutangaza utalii wa mazingira,mito inayoteteresha maji,misitu na vinginevyo.

Warembo hao kwa wakiwa katika hifadhi ya msitu asili wa Amani wamepata nafasi ya kuelezwa vivutio vinavyopatikana na hasa vinyonga wa pembe tatu ambao wanapatikani katika hifadhi hiyo.

Kwa upande wa warembo hao wamefurahishwa kutembelea hifadhi hiyo kwani wamepata nafasi ya kushuhudia vivutio mbalimbali vya utali

Kwa kukumbusha mashindano ya Miss Tanzania yanatarajia kufanyika Septemba 8 mwaka huu jijini Dar es Salaam.


Hivyo makala DC PANGANI AWATAKA WASHIRIKI WA MISS TANZANIA KUTANGAZA UTALII

yaani makala yote DC PANGANI AWATAKA WASHIRIKI WA MISS TANZANIA KUTANGAZA UTALII Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC PANGANI AWATAKA WASHIRIKI WA MISS TANZANIA KUTANGAZA UTALII mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/dc-pangani-awataka-washiriki-wa-miss.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DC PANGANI AWATAKA WASHIRIKI WA MISS TANZANIA KUTANGAZA UTALII"

Post a Comment