title : TTB YAINADI “ 787-8 DREAMLINER“ NCHINI INDIA
kiungo : TTB YAINADI “ 787-8 DREAMLINER“ NCHINI INDIA
TTB YAINADI “ 787-8 DREAMLINER“ NCHINI INDIA
Bodi ya Utalii Tanzania inaendele na mkakati wake wa kupenya katika masoko ya utalii ya Bara la Asia kwa lengo la kuongeza idadi ya watalii kutoka katika bara hilo pamoja na kuwashawishi watalii kuifanya Tanzania kuwa ni chaguo namba moja la utalii barani Afrika ”Tanzania, the leading and preferred tourist destination in Africa”, ambapo TTB imetayarisha maonesho matatu yatakayowahusisha wadau mbalimbali wa utalii wa nchini India.
Katika maonesho hayo yaliyoanza leo tarehe 17/9/2018 Mijini Delhi, The Roseate Aero City yametoa fursa kwa wadau wa utalii wa India kuvijuwa vivutio vya utalii vya Tanzania pamoja na kutangaza safari mpya za shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa kutumia ndege yake aina ya 787-8 Dreamliner mwezi November, 2018 inatarajia kuanzaisha safari za moja kwa moja kutoka Tanzania kwenda Mumbai nchini India.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB, Bi Devota Mdachi amesema “kupitia maonesho haya wadau wa utalii wa India watapata fursa ya kujuwa kwa kina kuhusu utalii wa Tanzania pamoja na kuweza kufanya biashara na wadau wa utalii wa Tanzania tuliyoambatana nao katika maonesho haya. Aidha, tunatarajia wadau hao wa India wataitumia ” 787-8 Dreamliner” ya ATCL kwa ajili ya kuwaleta watalii Tanzania, juhudi zinazofanywa na serikali ya Tanzania kupitika mashirika haya zitaongeza idadi ya watalii kutoka soko la utalii la India”.
Tarehe 19/09/2018 TTB itaendelea na maonesho hayo katika mji wa Ahmadabad, Crowne Plaza na tarehe 21/09/2018 maonesho yatafanyika mijini Mumbai, Hotel Orchid Mwaka 2017 Tanzania ilipokea idadi ya watalii 39,115 kutoka india.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa BOdi ya Utalii Tanzania, Bi. Devota Mdachi akikoa maelezo ya utalii wa Tanzania kwa wadau wa utalii wa India.
Wahishiriki wa onesho wakifuatika maelezo yanayotolewa ma mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bi. Devota Mdachi.
Mkurugenzi wa TTB, akitoa akifafanua jambo kwa wadau wa utalii wa India.
Hivyo makala TTB YAINADI “ 787-8 DREAMLINER“ NCHINI INDIA
yaani makala yote TTB YAINADI “ 787-8 DREAMLINER“ NCHINI INDIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TTB YAINADI “ 787-8 DREAMLINER“ NCHINI INDIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/ttb-yainadi-787-8-dreamliner-nchini.html
0 Response to "TTB YAINADI “ 787-8 DREAMLINER“ NCHINI INDIA"
Post a Comment