Biteko Asisitiza Sekta za kiserikali Kupunguza Urasimu, Kuondoa Rushwa

Biteko Asisitiza Sekta za kiserikali Kupunguza Urasimu, Kuondoa Rushwa - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Biteko Asisitiza Sekta za kiserikali Kupunguza Urasimu, Kuondoa Rushwa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Biteko Asisitiza Sekta za kiserikali Kupunguza Urasimu, Kuondoa Rushwa
kiungo : Biteko Asisitiza Sekta za kiserikali Kupunguza Urasimu, Kuondoa Rushwa

soma pia


Biteko Asisitiza Sekta za kiserikali Kupunguza Urasimu, Kuondoa Rushwa

Ni baada ya kubaini ucheleweshaji wa utoaji vibali vya uwekezaji sekta ya madini.

Na Nuru Mwasampeta, Geita.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kutoa kibali kwa wamiliki wa Kiwanda cha Kuchenjua Dhahabu kinacho milikiwa na kampuni ya Pedalu ili waweze kupewa leseni na kuendelea na shughuli ya kuchenjua madini hayo.

Biteko aliyasema hayo wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la kiwanda cha kuchenjua dhahabu kinachomilikiwa na kampuni ya wazawa ya Pedalu, katika kijiji cha Lumasa mjini Chato, iliyofanyika Desemba 2, 2019.

Alisema kuwa, kibali kingine kinapaswa kutolewa na Mkemia Mkuu wa Serikali na kubainisha kuwa, baada ya hafla hiyo atawasiliana naye ili awezeshe upatikanaji wa kibali hicho kwa lengo la kuiwezesha wizara ya madini kuendelea na mchakato wa kuandaa leseni itakayowaruhusu wawekezaji hao wazawa kuendelea na kazi ya uchenjuaji wa adini.“Jamani, Rais anataka viwanda, isitokee mtu hapa katikati anaweka urasimu na kuchelewesha azma ya Rais wetu, nchi hii tunaondoa urasimu tunataka kuondoa na rushwa,” alisisitiza Biteko.

Aidha, alibainisha kuwa, miongoni mwa masuala yanayowakimbiza wawekezaji nchini ni mawili tu, rushwa na urasimu na wala si sheria, na kusema kuwa, vitu hivyo ni kikwazo kikubwa katika kutimiza azma ya Serikali ya Tanzania ya Viwanda.

Aliwapongeza wawekezaji katika kiwanda cha Pedalu kwa kufanya uwekezaji huo mkubwa kwani anaamini madini yatakayopatikana kutoka katika kiwanda hicho yataiwezesha serikali kupata  kodi stahiki. Pia, Biteko aliwaomba wawekezaji hao wazawa kujenga viwanda vingine kama hivyo katika maeneo tofauti na kuahidi kupeleka wadau wenye nia ya kujifunza ili waweze kupata ujuzi wa namna ya kuwekeza ili kukuza sekta ya madini kwa pamoja.


Naibu Waziri wa Madini (kulia) na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (Kushoto) wakifungua kitambaa katika jiwe la msingi ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa kiwanda hicho cha kuchenjua dhahabu kilichopo mkoani Geita wilaya ya Chato mnamo tarehe 02 Januari, 2019.

????????????????????????????????????


Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (Kushoto) akisalimiana na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato  Dkt. Medard Kalemani (kulia) mara baada ya kuwasili katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwenye kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Pedalu kilichopo wilayani Chato mkoani Geita.
TWO
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (Wa tatu kutoka Kushoto), Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato Dkt. Medard Kalemani (wa pili kutoka kulia) wakielekea eneo maalum kwa ajili ya kupata maelezo pamoja na kuweka rasmi jiwe la msingi la kiwanda cha Pedalu uliofanyika tarehe 02 Januari, 2019 mjini Chato.
THREE
Msimamizi wa kiwanda cha kuchakata dhahabu cha Pedalu mjini Chato akitoa maelezo ya namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi ya uchenjuaji wa dhahabu kwa Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko na wajumbe alioambatana nao wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>




Hivyo makala Biteko Asisitiza Sekta za kiserikali Kupunguza Urasimu, Kuondoa Rushwa

yaani makala yote Biteko Asisitiza Sekta za kiserikali Kupunguza Urasimu, Kuondoa Rushwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Biteko Asisitiza Sekta za kiserikali Kupunguza Urasimu, Kuondoa Rushwa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/biteko-asisitiza-sekta-za-kiserikali.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Biteko Asisitiza Sekta za kiserikali Kupunguza Urasimu, Kuondoa Rushwa"

Post a Comment