title : AGIZO LATOLEWA KWA WANAOJENGA JENGO LA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KUENDELEA KULIPWA KWA WAKATI
kiungo : AGIZO LATOLEWA KWA WANAOJENGA JENGO LA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KUENDELEA KULIPWA KWA WAKATI
AGIZO LATOLEWA KWA WANAOJENGA JENGO LA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KUENDELEA KULIPWA KWA WAKATI
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, amemtaka mkandarasi SUMA JKT anayejenga jengo la wizara hiyo katika Mji wa Serikali Jijini Dodoma, kuhakikisha anaendelea kuwalipa wafanyakazi wanaojenga jengo hilo kwa wakati pamoja na kuhakikisha ubora wa jengo hilo unaendana na thamani hali pesa.
Mhe. Ulega amesema hayo leo (04.01.2019) mara baada ya kufika katika mji huo uliopo Kata ya Mtumba, kwa ajili ya kufanya tathmini ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la awali la Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kuonesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi inavyoendelea na kumtaka mkandarasi kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
“Unamlipa mtu kabla jasho lake halijakauka palepale unakuwa tayari umeshampa ndiyo dini inavyosema, ni jambo jema sana maana hawa mafundi wanasema wanalipwa kwa wakati, sisi muda wowote tutakuwa tunakuja hapa tunataka hii kazi imalizike kwa wakati na kwa viwango” Amesema Mhe. Ulega.
Mhe. Ulega amefafanua kuwa siyo jambo jema endapo kutatokea taarifa mara baada ya kumalizika kwa mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kuwa wafanyakazi waliokuwa wakijenga jengo hilo wanamdai mkandarasi ilhali wizara imemlipa pesa zote mkandarasi huyo SUMA JKT ili aweze kufanya kazi kwa wakati.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akipewa maelezo ya ujenzi wa jengo la wizara na Mkandarasi Msimamizi wa SUMA JKT Injinia David Pallangyo, katika Mji wa Serikali Jijini Dodoma
Baadhi ya wafanyakazi wanaojenga jengo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Mji wa Serikali Jijini Dodoma wakiendelea na hatua mbalimbali za ujenzi wa jengo hilo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala AGIZO LATOLEWA KWA WANAOJENGA JENGO LA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KUENDELEA KULIPWA KWA WAKATI
yaani makala yote AGIZO LATOLEWA KWA WANAOJENGA JENGO LA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KUENDELEA KULIPWA KWA WAKATI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AGIZO LATOLEWA KWA WANAOJENGA JENGO LA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KUENDELEA KULIPWA KWA WAKATI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/agizo-latolewa-kwa-wanaojenga-jengo-la.html
0 Response to "AGIZO LATOLEWA KWA WANAOJENGA JENGO LA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KUENDELEA KULIPWA KWA WAKATI"
Post a Comment