title : "Sipo tayari kuona Kigamboni inakuwa ya mapori,mimi sio mkuu wa wilaya wa kulinda mapori" DC Kigamboni.
kiungo : "Sipo tayari kuona Kigamboni inakuwa ya mapori,mimi sio mkuu wa wilaya wa kulinda mapori" DC Kigamboni.
"Sipo tayari kuona Kigamboni inakuwa ya mapori,mimi sio mkuu wa wilaya wa kulinda mapori" DC Kigamboni.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni mheshimiwa Sarah Msafiri amefanya ziara katika kata ya Pemba mnazi iliyomkutanisha na viongozi mbalimbali na wananchi wa kata hiyo akiwa na lengo la kujuana nao,kupata taarifa ya maendeleo na changamoto zilizopo katika kata hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo amesema amegundua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kata hiyo ikiwemo ya uwepo wa maeneo yenye mapori ambayo hayajaendelezwa na wamiliki wa maeneo hayo yanayopelekea kuwepo kwa wanyama pori katika maeneo hayo ambao wanaharibu mazao ya wananchi.
Hivyo amewataka viongozi wa kata hiyo kumuandalia orodha ya ya wamiliki waliowekeza katika maeneo hayo ambayo yameendelezwa na yasiyoendelezwa na orodha ya wanyama pori waliopo ili kuondoa maeneo yasiyoendelezwa.
"Sipo tayari kuona Kigamboni inakuwa ya mapori,mimi sio mkuu wa wilaya wa kulinda mapori" amesema mkuu wa wilaya.
Kwa upande mwingine mkuu wa wilaya amewataka maafisa mipango miji kukutana na wananchi na kuwapa elimu kuhusiana na nyumba zilnazopigwa X (zilizo karibu na barabara)zipi zinazitakiwa kulipwa na zipi hazitakiwi kulipwa kufuatiwa na sheria zilizowekwa na wizara husika.
Pia ametoa siku nne kwa afisa mipango miji wa wilaya ya Kigamboni kufuatilia ujenzi unaoendelea katika kituo watoto yatima( dunia ya heri) katika mtaa wa puna center kama wanakibali.
Aidha amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa viongozi wa mitaa kuwapa taarifa ya wahamiaji haramu wasiokuwa na vibali katika maeneo yao.
Pia amewapongeza vijana wa kata hiyo kwa kutoa ushirikaino kwa katika oparesheni iliyofanyika ya kukamata wavuvi haramu na kupiga vita uvuvi haramu katika maeneo hayo ya fukwe za bahari.
Manispaa imetenga pesa kwa ajili ya kuwakopesha vikundi vya kina mama na vijana kwa lengo la kufanyia biashara ili kujikwamua kiuchumi .
Hivyo amewataka vijana kuacha kucheza michezo ya bahati nasibu na kufanya kazi na kujiunga katika vikundi mbalimbali vyenye maendeleo.
Hivyo makala "Sipo tayari kuona Kigamboni inakuwa ya mapori,mimi sio mkuu wa wilaya wa kulinda mapori" DC Kigamboni.
yaani makala yote "Sipo tayari kuona Kigamboni inakuwa ya mapori,mimi sio mkuu wa wilaya wa kulinda mapori" DC Kigamboni. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala "Sipo tayari kuona Kigamboni inakuwa ya mapori,mimi sio mkuu wa wilaya wa kulinda mapori" DC Kigamboni. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/sipo-tayari-kuona-kigamboni-inakuwa-ya.html
0 Response to ""Sipo tayari kuona Kigamboni inakuwa ya mapori,mimi sio mkuu wa wilaya wa kulinda mapori" DC Kigamboni."
Post a Comment