Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Miradi ya Kijamii na Kufuatilia Changamoto Zinazowakabili Wananchi Katika Utekelezaji Miradi Hiyo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Miradi ya Kijamii na Kufuatilia Changamoto Zinazowakabili Wananchi Katika Utekelezaji Miradi Hiyo. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Miradi ya Kijamii na Kufuatilia Changamoto Zinazowakabili Wananchi Katika Utekelezaji Miradi Hiyo., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Miradi ya Kijamii na Kufuatilia Changamoto Zinazowakabili Wananchi Katika Utekelezaji Miradi Hiyo.
kiungo : Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Miradi ya Kijamii na Kufuatilia Changamoto Zinazowakabili Wananchi Katika Utekelezaji Miradi Hiyo.

soma pia


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Miradi ya Kijamii na Kufuatilia Changamoto Zinazowakabili Wananchi Katika Utekelezaji Miradi Hiyo.





Na.Othman Khamis OMPR.
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Wanafunzi wanaweza kuwa Watumishi wazuri wa Serikali, Taasisi, Mashirika ya Umma na hata Sekta  Binafsi endapo wataamua kuzingatia mafunzo wanayopewa wakati wanapotafuta Elimu.
Alisema utumishi utakaotukuka wa Kikazi hicho cha sasa utazidi kuleta faida na neema kama pia Wanafunzi hao watafuata malezi bora ya Majumbani na hata Mitaani kwa vile sehemu kubwa ya malezi yao yanategemewa kupatikana kwa Wazazi wao.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati alipofanya ziara fupi ya kukagua maendeleo ya miradi tofauti ya Kijamii pamoja na kufuatilia changamoto zinazowakabili Wananchi katika uendelezaji wa Miradi hiyo ndani ya Jimbo analoliongoza la Mahonda liliomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B”.
Alisema utafiti unaonyesha wazi kwamba Watoto wengi wamebarikiwa kuwa na akili nyingi za kutosha Kimasomo lakini kinachokosekana ndani ya Jamii katika kuwaendeleza Watoto hao ni ushirikiano wa karibu kati ya Walimu na Wazazi katika baadhi ya Maeneo Nchini.
Balozi Seif alieleza kwamba katika suala zima la kumuandaa Mtoto katika mazingira salama ya kupata malezi sambamba na Taaluma Wazazi wanaendelea kubeba dhima ya kufuatilia nyendo za Watoto wao hasa katika vipindi vya masomo ya ziara kwa nyakati za Jioni au usiku.
Alisema nyakati hizo za ziada mara nyingi  huonekana kutoa mwanya kwa baadhi ya Wanafunzi watukutu kufanya vitendo vilivyo nje ya Maadili yao na matokeo yake wengine huishia kupata Mimba za Utotoni jambo linalowasababishia kuacha kuendelea na masomo yao.
Kwa upande wa Walimu Balozi Seif  aliwakumbusha kuwasiliana na Wazazi wa wanafunzi pale wapothibitisha uwepo wa Tabia chafu za Mwanafunzi wakati wa masomo yao madarasani.
Katika ziara hiyo Mwakilishi huyo wa Jimbo la Mahonda alikagua Tangi la Maji safi na Salama liliopo katika Skuli ya Msingi ya Mangapwani na kuushauri Uongozi wa Hamashauri ya Wilaya ya Kaskazini “B”  kuangalia uwezekano wa kuwekwa kwa Tangi jengine kubwa la Maji ili kukidhi mahitaji ya Wanafunzi, Walimu pamoja na Baadhi ya Wananchi wanaoizunguuka Skuli hiyo.
Baadae Balozi Seif akakagua maendeleo ya Ujenzi wa Jengo Jipya lililolengwa kutumiwa na Wanafunzi wa Skuli ya  Maandalizi  ya Vuga Mkadini  kwa masomo ya Msingi hapo baadae na kuona Tangi la Maji ambalo kwa sasa linahitaji kuwekwa jengine kubwa kutokana na mahitaji zaidi ya Wananchi.
Balozi Seif aliwaeleza Wananchi wa Shehia hiyo ya Vuga Mkadini kwamba Uongozi wa Jimbo la Mahonda utashirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “B” katika kuongeza nguvu za kukamilishwa kwa Jengo hilo kwa hatua ya Kifusi, Plasta na Saruji.
Akilikagua Daraja lililojengwa katika Bonde la  Matetema  ambalo litasaidia kuondosha usumbufu kwa Wananchi wa Ng’ambo ya Kazole Mwakilishi huyo wa Jimbo la Mahonda  aliwatahadharisha Viongozi wanaosimamia miradi ya Kijamii kuwa makini na Makandarasi wababaishaji.
Balozi Seif alisema miradi mingi ya Kijamii Majimboni huzorota au mengine kufifia kabisa kutokana na baadhi ya Viongozi kuwapa jukumu hiyo jamaa na marafiki zao kwa nia ya kumsaidia riziki lakini hatma yake hakuna kinachozingatiwa katika ukamilishwaji wa miradi hiyo kutokana na Ujamaa uliotawala katika mkazi hizo za Kijamii.


Hivyo makala Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Miradi ya Kijamii na Kufuatilia Changamoto Zinazowakabili Wananchi Katika Utekelezaji Miradi Hiyo.

yaani makala yote Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Miradi ya Kijamii na Kufuatilia Changamoto Zinazowakabili Wananchi Katika Utekelezaji Miradi Hiyo. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Miradi ya Kijamii na Kufuatilia Changamoto Zinazowakabili Wananchi Katika Utekelezaji Miradi Hiyo. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/makamu-wa-pili-wa-rais-wa-zanzibar-mhe_2.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Miradi ya Kijamii na Kufuatilia Changamoto Zinazowakabili Wananchi Katika Utekelezaji Miradi Hiyo."

Post a Comment