KONDO AMUUA MKEWE KISA KUCHAT NA SIMU-RPC WANKYO

KONDO AMUUA MKEWE KISA KUCHAT NA SIMU-RPC WANKYO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KONDO AMUUA MKEWE KISA KUCHAT NA SIMU-RPC WANKYO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KONDO AMUUA MKEWE KISA KUCHAT NA SIMU-RPC WANKYO
kiungo : KONDO AMUUA MKEWE KISA KUCHAT NA SIMU-RPC WANKYO

soma pia


KONDO AMUUA MKEWE KISA KUCHAT NA SIMU-RPC WANKYO

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
JESHI la polisi Mkoani Pwani ,limefanikiwa kumkamata Salum Mzee Kondo (38),fundi ujenzi mkazi waKidongoChekundu ,Bagamoyo aliyehusika na tukio la mauaji ya mkewe Mwajuma Omary (27) kisha kutoroka baada ya kutenda kosa hilo.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa septemba 2 mwaka huu ,Yombo Buza jijini Dar es salaam ambako alikimbilia baada ya kufanya kitendo hicho Agosti 31 2018, saa 9 alasiri huko Kidongochekundu.

Akiweka bayana kuhusiana na tukio hilo kwa waandishi wa habari ,kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa alisema, mtuhumiwa alipokamatwa alikiri kutenda kosa hilo ,na kudai alichukua hatua hiyo kutokana na wivu wa kimapenzi .

Alieleza kwamba , mkewe alikuwa akichat na simu huku akiwa anacheka mwenyewe ndipo alipoamua kumnyang'anya simu na kukuta message alizokuwa akichat na mwanaume mwingine .

"Jambo hilo lilisababisha mgogoro kati yao ,ambao ulisuluhishwa na mwenyekiti wa kitongoji cha Magomeni B, lakini marehemu alishikilia kuchoshwa kuishi na mumewe huyo na kuomba kupewa talaka na mumewe aligoma kutoa talaka " alifafanua Nyigesa .

Pamoja na hilo ,Nyigesa alisema wawili hao walikuwa na mgogoro mwingine, uliotokana na mtuhumiwa kuchukua ATM Card ya marehemu mkewe na kwenda kutoa sh.50,000 bila ridhaa yake.

Alibainisha ,jambo hilo lilimsababisha marehemu mkewe kuondoka nyumbani wanakoishi na kwenda kuishi kwa baba yake mdogo.

Kamanda huyo alieleza ,ilipofika tarehe 31 agost mwaka huu alimpigia simu mumewe kuhitaji fedha zake hizo ambapo mumewe alimwambia aende nyumbani kwao akachukue na mkewe huyo (marehemu)aliendelea kushikilia kutaka fedha zake na talaka ndipo mtuhumiwa kwa hasira alimkaba na kumsababisha kifo .

Baada ya kutenda kosa hilo mtuhumiwa alimfunika marehemu kwa shuka ndani ya chumba walichokuwa wakiishi na kuacha ujumbe kuwa ameua kutokana na wivu wa kimapenzi .

Kwa mujibu wa Nyigesa ,Ujumbe huo uliendelea kueleza ,mtuhumiwa nae anaenda kujiua hivyo mali zote walizoacha ni za watoto wawili waliozaa na marehemu .



Hivyo makala KONDO AMUUA MKEWE KISA KUCHAT NA SIMU-RPC WANKYO

yaani makala yote KONDO AMUUA MKEWE KISA KUCHAT NA SIMU-RPC WANKYO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KONDO AMUUA MKEWE KISA KUCHAT NA SIMU-RPC WANKYO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/kondo-amuua-mkewe-kisa-kuchat-na-simu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KONDO AMUUA MKEWE KISA KUCHAT NA SIMU-RPC WANKYO"

Post a Comment