JESHI LA POLISI MKOA WA TABORA LAMKAMATA FUNDI NA MMILIKI WA KIWANDA KIDOGO CHA KUTENGENEZA SILAHA HARAMU

JESHI LA POLISI MKOA WA TABORA LAMKAMATA FUNDI NA MMILIKI WA KIWANDA KIDOGO CHA KUTENGENEZA SILAHA HARAMU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JESHI LA POLISI MKOA WA TABORA LAMKAMATA FUNDI NA MMILIKI WA KIWANDA KIDOGO CHA KUTENGENEZA SILAHA HARAMU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JESHI LA POLISI MKOA WA TABORA LAMKAMATA FUNDI NA MMILIKI WA KIWANDA KIDOGO CHA KUTENGENEZA SILAHA HARAMU
kiungo : JESHI LA POLISI MKOA WA TABORA LAMKAMATA FUNDI NA MMILIKI WA KIWANDA KIDOGO CHA KUTENGENEZA SILAHA HARAMU

soma pia


JESHI LA POLISI MKOA WA TABORA LAMKAMATA FUNDI NA MMILIKI WA KIWANDA KIDOGO CHA KUTENGENEZA SILAHA HARAMU

NA  TIGANYA VINCENT RS TABORA.
JESHI la Polisi Mkoani Tabora linamsikilia mkazi wa kijiji cha Kinamagi Kata ya Kigwa wilayani Uyui Mrisho Juma (44) kwa tuhuma za kumiliki kiwanda cha Kutengeneza silaha za kienyeji  aina ya Gobore.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Emmanuel Nley imesema kuwa Juma alikamatwa Septemba 02 mwaka huu  nyumbani kwake akiendelea na utengenezaji wa silaha hizo.

Kamanda Nley alisema kuwa mtuhumiwa alikutwa na gobore tatu akiendelea kuzitengeneza pamoja na bastola moja ikiwa imekamilika.

Alisema kuwa hata watuhumiwa ambao wamekuwa wakimatwa na gobore wamekuwa wakidai kununua kwake na ndipo Jeshi la Polisi liliweka mtego na kumukamata Kwa mujibu wa Kamanda  Nley baada ya kumhoji mtuhumiwa alikiri  kuwa ndiye mtengenezaji wa silaha hizo na uziuza maeneo mbali mbali mkoani hapa.

Kufuatia tukio hilo Kamanda wa Polisi ametoa wito kwa wananchi ambao wanamiliki silaha bila kufuata utaratibu wajisalimishe kabla hatua kali dhidi yao hajachukuliwa.

Wakati huo huo Kamanda huyo amesema kuwa Jeshi hilo linaendelea kuwashikilia Askari Polisi kumi(10) wa Wilaya ya Igunga wakihusishwa na kifo cha Selemani Jumapili  waliyekuwa wamemkamata kwa mahojiano.

Nley amesema kuwa Wataalamu kutoka Makao Makuu wa Jeshi hilo wanaendelea na mahojiano na askari hao na uchunguzi ukikamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kuhusika na tukio hilo.

Aliongeza kuwa mwili wa marehemu Jumapili ulifanyiwa uchunguzi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora na taarifa ya matokeo itatolewa Mahakamani.

Alisema Jumapili alikamatwa na Polisi hao waliokuwa katika misako Agosti 29 saa nane mchana  na baadaye akiwa katika Kituo cha Polisi alionekana mgonjwa na kukimbizwa Hospitali na ilipofika saa tano usiku alifariki wakati akipata matibabu kwenye hosptali ya wilaya Igunga alipokuwa akipata matibabu.


Hivyo makala JESHI LA POLISI MKOA WA TABORA LAMKAMATA FUNDI NA MMILIKI WA KIWANDA KIDOGO CHA KUTENGENEZA SILAHA HARAMU

yaani makala yote JESHI LA POLISI MKOA WA TABORA LAMKAMATA FUNDI NA MMILIKI WA KIWANDA KIDOGO CHA KUTENGENEZA SILAHA HARAMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JESHI LA POLISI MKOA WA TABORA LAMKAMATA FUNDI NA MMILIKI WA KIWANDA KIDOGO CHA KUTENGENEZA SILAHA HARAMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/jeshi-la-polisi-mkoa-wa-tabora.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "JESHI LA POLISI MKOA WA TABORA LAMKAMATA FUNDI NA MMILIKI WA KIWANDA KIDOGO CHA KUTENGENEZA SILAHA HARAMU"

Post a Comment