title : Wananchi wakimiliki nyumba ni maendeleo ya Kiuchumi
kiungo : Wananchi wakimiliki nyumba ni maendeleo ya Kiuchumi
Wananchi wakimiliki nyumba ni maendeleo ya Kiuchumi
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mkurugenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) AlexenderNg'winamila, amesema kuwa mikopo ya nyumba kwa wananchi ikitolewa na wananchi hao wakamiliki nyumba hizo ni maendeleo katika ukuaji wa uchumi.
Alexander aliyasema hayo wakati akizindua kozi ya mafunzo kwa wafanyakazi benki kuhusiana utoaji wa mikopo ya nyumbani kwa wananchi.
Amesema kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda umiliki wa nyumba ni muhimu kwa kufanya wananchi wanaofanya uchumi huo kuwa na makazi bora.
Alexander amesema kuwa Taasisi ya Benki Nchini (TIOB) kwa kushirikiana Taasisi ya Utoaji wa Mikopo ya Nyumba (TMRC) katika kuandaa kozi fupi kwa ajili ya wafayakazi wa Benki kupata mbinu katika utoaji wa mikopo ya nyumba.Aidha amesema kuwa baada ya mafunzo hayo benki zikifanya kwa ufanisi zitaongeza wateja wa mikopo ya nyumba.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Ocar Mgaya amesema mafunzo hayo yalishatolewa katika chuo cha BOT cha mwanza kwa wafanyakazi 300.Katika utoaji mikopo taasisi kulikuwa na changamoto kwa kutoa baadhi ya taasisi lakini tumeanza kutoa kwa taasisi zote za fedha ziweze kupesha mikopo ya nyumba.
Mkurugenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT)Alexender Ng'winamila akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya utoaji mikopo ya nyumba kwa watumishi wa taasisi za fedha uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Ocar Mgaya akizungumza kuhusiana na utaoji wa mikopo ya benki kwa ajili ya ukopeshaji wa mikopo ya nyumba kwa wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi za Benki Nchini (TIOB) Patrick Mususa akizungumza juu ya uandaji wa mafunzo kwa wafanyakazi wa benki katika utoaji wa mikopo ya nyumba kwa wananchi.
Hivyo makala Wananchi wakimiliki nyumba ni maendeleo ya Kiuchumi
yaani makala yote Wananchi wakimiliki nyumba ni maendeleo ya Kiuchumi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wananchi wakimiliki nyumba ni maendeleo ya Kiuchumi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/wananchi-wakimiliki-nyumba-ni-maendeleo.html
0 Response to "Wananchi wakimiliki nyumba ni maendeleo ya Kiuchumi"
Post a Comment