title : Serikali Kuajiri Walimu 2000 wa Masomo ya Sayansi-Naibu waziri Kakunda
kiungo : Serikali Kuajiri Walimu 2000 wa Masomo ya Sayansi-Naibu waziri Kakunda
Serikali Kuajiri Walimu 2000 wa Masomo ya Sayansi-Naibu waziri Kakunda
Na. Ofisa Habari Mufindi
Naibu Waziri Ofisi ya Rais (OR-TAMISEMI) Mhe Joseph Kakunda, amesema serikali ipo katika hatua a mwisho kukamilisha mchakato wa kuajiri waalimu 2000 wa masomo ya sayansi ili kupunguza changamoto ya uchache wa walimu wa kada hiyo katika shule za umma nchini
Mhe. Kakunda ameyasema hayo katika shule kongwe ya Sekondari Mdabulo, akiwa kwenye ziara ya kikazi Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, baada ya Mkuu wa shule hiyo Bw. George Mgomba, kueleza changamoto ya uhaba wa walimu wa sayansi katika shule yake.
“Serikali kwa mwaka huu inaendelea na mchakato wa kuajiri walimu wa sayansi wapatao 2000 hivyo, taarifa yenu naichukua mwenyewe na kuipeleka kwa Mhe. Waziri Jafo, bila shaka walimu wawili 02 mnaowahitaji katika shule yenu mtawapata na hili nalibeba kwa ajili ya utekelezaji” alisisitiza Waziri Kakunda
Aidha, Mhe. Kakunda ameridhishwa na majengo mapya ya Shule hiyo iliyojengwa kwa mfumo wa “Force Account” kwa kuzingatia maelekezo ya kitaifa baada ya kujionea madarasa na mabweni mazuri hivyo, amesisitiza utaratibu uliotumika wa kujenga kwa njia ya Force Account uendeleee hata wakati wa mradi wa ujenzi wa mabweni utakapoanza, ambapo serikali tayari imetenga Jumla ya Tsh Milioni 100 kwa shule ya Sekondari Mdabulo.

Naibu waziri Kakunda, akiongozwa na Mkuu wa shule ya Sekondari Mdabulo kukagua madarasa na mabweni mapya yaliyojengwa Serikali

Hivyo makala Serikali Kuajiri Walimu 2000 wa Masomo ya Sayansi-Naibu waziri Kakunda
yaani makala yote Serikali Kuajiri Walimu 2000 wa Masomo ya Sayansi-Naibu waziri Kakunda Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali Kuajiri Walimu 2000 wa Masomo ya Sayansi-Naibu waziri Kakunda mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/serikali-kuajiri-walimu-2000-wa-masomo.html
0 Response to "Serikali Kuajiri Walimu 2000 wa Masomo ya Sayansi-Naibu waziri Kakunda"
Post a Comment