title : Mkurugenzi Mtendaji TIC aongoza msafara wa wadau wa Serikali na Sekta binafsi kwenda nchini Korea kwa ziara ya kikazi
kiungo : Mkurugenzi Mtendaji TIC aongoza msafara wa wadau wa Serikali na Sekta binafsi kwenda nchini Korea kwa ziara ya kikazi
Mkurugenzi Mtendaji TIC aongoza msafara wa wadau wa Serikali na Sekta binafsi kwenda nchini Korea kwa ziara ya kikazi
Balozi Massuka akimkaribisha nchini Korea Bw.Adonis Bitegeko ambaye ni Mkurugenzi wa Udhibiti na Mwakilishi Wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Chakula Tanzania (TFDA), moja ya taasisi muhimu za serikali zinazoshiriki katika ziara hiyo ya uhamasishaji viwanda nchini Korea. Anayeshuhudia ni Bw.Francis Mossongo, Afisa Uchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Tanzania.
Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Dawa na Vifaa Tiba Nchini (Tanzania Association of Phramaceutical Industry, TAPI), Bw.Abbas S.Mohamed, ambaye pia ni Mkurugenzi Wa Kampuni ya Samiro Pharmaceuticals Ltd ya jijini Dar es Salaam, akipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon Seoul na Mhe. Matilda S.Massuka, Balozi Wa Tanzania nchini Korea. TAPI inashirikiana na Serikali katika kufanikisha malengo ya ziara hiyo Nchini Korea na China, wakiiwakilisha Sekta Binafsi ya Tasnia ya Dawa na Vifaa Tiba ya nchini Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Korea, Mhe.Matilda S. Massuka, akimkaribisha Bw. Asgaral Alimohamed, Mwanachama Wa TAPI na Mkurugenzi Mtendaji Wa Kampuni ya Mwafrika Pharmaceutical Ltd ya jijini Tanga, baada ya kutambulishwa kwake na Bw.Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC anayeongoza ujumbe wa Tanzania, nchini humo.
Balozi wa Tanzania nchini Korea Matilda Massuka akiulaki na kuukaribisha ujumbe wa Tanzania uliowasilini Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Seoul Incheon, nchini Korea kwa ajili ya ziara ya uhamasishaji uwekezaji na biashara katika sekta ya Dawa na Vifaa Tiba nchini Tanzania. Katika hatua ya awali, Ujumbe huo unaongozwa na Bw.Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, huku Ummy Mwalimu Waziri wa Afya wa Tanzania akitarajiwa kuungana na ujumbe huo nchini Korea mapema kesho kwa zaira ya kikazi ya siku tano (5) kuanzia Agosti 11 hadi15 mwaka huu
Hivyo makala Mkurugenzi Mtendaji TIC aongoza msafara wa wadau wa Serikali na Sekta binafsi kwenda nchini Korea kwa ziara ya kikazi
yaani makala yote Mkurugenzi Mtendaji TIC aongoza msafara wa wadau wa Serikali na Sekta binafsi kwenda nchini Korea kwa ziara ya kikazi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mkurugenzi Mtendaji TIC aongoza msafara wa wadau wa Serikali na Sekta binafsi kwenda nchini Korea kwa ziara ya kikazi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mkurugenzi-mtendaji-tic-aongoza-msafara.html
0 Response to "Mkurugenzi Mtendaji TIC aongoza msafara wa wadau wa Serikali na Sekta binafsi kwenda nchini Korea kwa ziara ya kikazi"
Post a Comment