NSSF yatakiwa kutoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Watanzania wote

NSSF yatakiwa kutoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Watanzania wote - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NSSF yatakiwa kutoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Watanzania wote, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NSSF yatakiwa kutoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Watanzania wote
kiungo : NSSF yatakiwa kutoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Watanzania wote

soma pia


NSSF yatakiwa kutoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Watanzania wote


Serikali imelitaka Shirika la Hifadhi ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii NSSF kutoa elimu zaidi kwa wananchi kuhusiana na faida za kujiunga katika hifadhi za jamii nchini. 

Hayo yameswemwa na Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Sera,Bunge,Ajira ,Vijana na Watu Wenye Ulemavu) Jenister Mhagama kwenye wiki ya Taifa ya maonesho ya wiki ya vijana yanayofanyika katika viwanja vya Tangamano mkoani Tanga ambapo amesema kuwa bado watanzania wengi hawana elimu ya kutosha kuhusiana na kujiwekea akiba ya uzeeni na faida zake hivyo NSSF inaoaswa kuhakikisha inatoe elimu hii. 

“Nawataka NSSF muhakikishe elimu hii mnaitoa ipasavyo na iwafikie watanzania wote nchini ,mwende vijijini huko muelekeze wananchi nao wapate uelewa wa hifadhi za jamii na faida zake”alisema Waziri Muhagama. Mhagama amesema kuwa NSSF ndio inajukumu sasa la kuandikisha wananchi walio kwenye sekta isiyo rasmi hivyo wahakikishe wanawafikia wananchi wengi waliopo kwenye sekta hiyo na hasa wa vijijini na kuwapatia uelewa na waweze kujiunga na kufaika na mafao yote ya NSSF. 

Kwa upande wake kaimu meneja wa NSSF mkoa wa TANGA ,Aisha Nyemba mpaka sasa wameendelea kutoa elimu kwa wananchi kujiandikisha katika mpango wa hiari ambao utawawezesha kufaidika na mafao mbali mbali ikiwemo mafao ya matibabu. Kwa mujibu wa Nyemba mpaka sasa NSSF imeandikisha vikundi vya wajasiriamali idadi ya 47 katika mpango wa hiari na wanachangia michango yao kila mwezi ambapo pia juhudi zinaendelea kuhakikisha wanafikia vikundi vingi vya wajasiriamali katika mkoa wa Tanga. 

Maonyesho haya ya Taifa ya wiki ya vijana yamefikia kilele chake oktoba 14 mwaka huu ambapo yataendana na sherehe za uzimaji wa mwenge kitaifa katika uwanja wa Mkwakwani na kuenzi miaka 19 ya kifo cha Rais wa kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 
 Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Sera,Bunge,Ajira ,Vijana na Watu Wenye  Ulemavu) Mhe. Jenister Mhagama, akipata maelezo namna ya kujiunga na uchangiaji wa hiari katika Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa maonesho ya Wiki ya Taifa ya Vijana yanayofanyika katika Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga 
Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Sera,Bunge,Ajira ,Vijana na Watu Wenye  Ulemavu) Mhe. Jenister Mhagama na Naibu Waziri Mhe. Anthony Mavunde, wakipata maelezo namna ya kujiunga na uchangiaji wa hiari katika Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa maonesho ya Wiki ya Taifa ya Vijana yanayofanyika katika Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga .


Hivyo makala NSSF yatakiwa kutoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Watanzania wote

yaani makala yote NSSF yatakiwa kutoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Watanzania wote Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NSSF yatakiwa kutoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Watanzania wote mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/nssf-yatakiwa-kutoa-elimu-ya-hifadhi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NSSF yatakiwa kutoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Watanzania wote"

Post a Comment