title : WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KANGI LUGOLA AMTIMUA KAMISHANA WA MAGEREZA KWENYE MKUTANO WAKE
kiungo : WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KANGI LUGOLA AMTIMUA KAMISHANA WA MAGEREZA KWENYE MKUTANO WAKE
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KANGI LUGOLA AMTIMUA KAMISHANA WA MAGEREZA KWENYE MKUTANO WAKE
*Pia awataka makamishina na wakuu wa Idara kumuonesha Ilani ya CCM
Na Said Mwishehe,Glubu ya jamii
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ameamua kumtimua katika kikao chake Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Kamishina Jenerali Dk.Juma Malewa kwasababu za kuchelewa kuingia mkutanoni.
Kabla ya kumtoa nje leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lugola alisema baada ya mkutano wake kuanza ni marufuku mtu yeyote kuingia ndani isipokuwa waandishi wa habari tu ndio watakaoruhusiwa.
Hivyo Dk. Malewa aliingia ukumbini saa tano na dakika tatu ambapo Waziri Lugola akamtaka atoke nje mara moja. Pamoja na Dk.Malewa kuomba msamaha kwa Waziri iliyoambatana na saluti alimkatalia na kumuamuru atoke nje ya ukumbi na hataki yeyote ambaye yupo chini yake na hajafika ni marufuku kuingia ndani.
Wakati huo huo kabla ya kuanza kikao hicho alitoa maagizo kwa Makamishina waliopo kwenye mkutano huo aliwataka kueleza milango yao inayoendana na Ilani ya CCM. "Nawaomba kila mmoja aoneshe Ilani ya CCM na ambaye hana anyooshe mkono juu na nitajua kama anayo au laa,"amesema Lugola.
Hata hivyo hakuna aliyekuwa nayo na hivyo akatangaza hata mkutano ambao alitaka kuufanya kati yake na Makamishina na Wakuu wengine wa Idara alisema ameuahirisha na kila mmoja akachukue Ilani yake ndio wafanye kikao.
Hivyo makala WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KANGI LUGOLA AMTIMUA KAMISHANA WA MAGEREZA KWENYE MKUTANO WAKE
yaani makala yote WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KANGI LUGOLA AMTIMUA KAMISHANA WA MAGEREZA KWENYE MKUTANO WAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KANGI LUGOLA AMTIMUA KAMISHANA WA MAGEREZA KWENYE MKUTANO WAKE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waziri-wa-mambo-ya-ndani-kangi-lugola_6.html
0 Response to "WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KANGI LUGOLA AMTIMUA KAMISHANA WA MAGEREZA KWENYE MKUTANO WAKE"
Post a Comment