title : KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AWAHIMIZA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUHAMASHA ARI YA UFANYAJI KAZI KWA WANANCHI.
kiungo : KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AWAHIMIZA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUHAMASHA ARI YA UFANYAJI KAZI KWA WANANCHI.
KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AWAHIMIZA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUHAMASHA ARI YA UFANYAJI KAZI KWA WANANCHI.
Na Raymond Mushumbusi WAMJW
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga amewaasa maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii nchini kuamsha ari ya kufanya kazi kwa wananchi ili kujiletea maendeleo.
Ameyasema hayo wakati alipokutana na kuzungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii mkoani Iringa alipokuwa akifanya ziara kujionea utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya jamii nchini.
Bibi Sihaba Nkinga ameongeza kuwa viongozi wa Halmashauri na Mikoa nchini wanatakiwa kuwapa nafasi Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii ili kurejesha ari ya wananchi kujitolea katika kutekeleza shhughuli za kimaendeleo katika maeneo yao.
“ Nawaomba Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii mtimize majukumu yenu ipasavyo ili kuamsha ari ya ufanyaji kazi kwa wananchi ili kuleta maendeleo katika maeneo yao” alisema Bibi Sihaba.
Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga pia amesisitiza matumizi ya rasilimali zilizopo ili kuendelea kuhimiza wananchi kujitolea katika kujitolea na kufanya kazi zitakazowaletea maendeleo katika maeneo yao.
Aidha kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bibi Waumoja Ayoub amemuakikishia Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga kuwapa ushirikiano Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii ili waweze kutimkiza majukumu yao.
“Sisi viongozi wa mkoa tupo tayari kutoa ushirikiano kwa Maafisa hawa ili kuwawezesha kutimiza majukumu yao kwa wakati na katika ufanisi” alisema Bibi Waumoja.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga amefanya ziara mkoani Iringa kwa lengo la kujionea utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii na kuamsha aerinya wananchi katika kujitolea kufanya kazi kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Hivyo makala KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AWAHIMIZA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUHAMASHA ARI YA UFANYAJI KAZI KWA WANANCHI.
yaani makala yote KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AWAHIMIZA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUHAMASHA ARI YA UFANYAJI KAZI KWA WANANCHI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AWAHIMIZA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUHAMASHA ARI YA UFANYAJI KAZI KWA WANANCHI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/katibu-mkuu-sihaba-nkinga-awahimiza.html
0 Response to "KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AWAHIMIZA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUHAMASHA ARI YA UFANYAJI KAZI KWA WANANCHI."
Post a Comment