TEMBO, NDEGE, CHATU NA UBUYU WAVUTIA MAELFU YA WATALII KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE

TEMBO, NDEGE, CHATU NA UBUYU WAVUTIA MAELFU YA WATALII KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TEMBO, NDEGE, CHATU NA UBUYU WAVUTIA MAELFU YA WATALII KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TEMBO, NDEGE, CHATU NA UBUYU WAVUTIA MAELFU YA WATALII KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE
kiungo : TEMBO, NDEGE, CHATU NA UBUYU WAVUTIA MAELFU YA WATALII KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE

soma pia


TEMBO, NDEGE, CHATU NA UBUYU WAVUTIA MAELFU YA WATALII KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE

Na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii, Tarangire
Maelfu ya watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani wanatembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire iliyo umbali wa kilometa 118  kutoka jiji la arusha katika barababra ya lami ya Arusha-Dodoma, na Kusini Mashariki mwa Ziwa Manyara. 
Jina la hifadhi hii yenye ukubwa wa kilomita za mraba 2,850 lina asili ya 
 Mto Tarangire unaotiririsha maji mwaka mzima kuelekea upande wa Kaskazini mwa hifadhi hii ndio umeipa hifadhii hii jina hilo, sababu ya uwepo wake katika kipindi chote cha mwaka ni msaada mkubwa kwa maisha ya wanyamapori ndani na nje ya hifadhii hii. 
Hifadhi hii ni maarufu kwa makundi makubwa ya tembo wakubwa na wenye pembe ndefu kuliko hifadhi nyingine nchini Tanzania. 
Pia inaongoza duniani kwa kuwa na tembo wengi kwenye eneo la kilometa za mraba, ambapo unaweza kuona kundi la tembo zaidi ya mia tano kwa mara moja. Hifadhi hii pia ina mandhari nzuri ya kuvutia inayotokana na maumbile ya mibuyu inayosadikiwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka elfu nane. 
Wanyama wa aina nyingi wanaopatikana ndani ya hifadhi hii ni pamoja na punda milia, nyumbu, swala, simba, nyati, kongoni, chui, duma na wengine wengi pamoja na aina 550 za ndege . Hifadhi hii ni maarufu katika ukanda wa kaskazini mwa Tanzania ambapo wengi, kutoka ndani na nje ya nchi kwani hupenda kutembelea hifadhi hii. 
Umaarufu mwingine wa hifadhi hii ni pamoja ya aina ya chatu walio na uwezo wa kukwea miti. Kutokana na umaarufu huu idadi ya wageni wanaotembelea hifadhi imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka. 
 Unaweza kutembelea hifadhi hii wakati wote wa mwaka na kuwaona wanyama wote bila matatizo kutokana na mazingira mazuri ya hifadhi yanayosaidiwa na Mto Tarangire unaokatiza katikati ya hifadhi. 
Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ina zaidi ya jamii 550 za ndege ambao ndio wamejulikana, na kati ya ndege hao baadhi yao wapo katika tishio la kutoweka. Tafiti zinaonyesha kwamba kipindi cha mvua ndio kipindi kizuri sana kwa aina nyingi za ndege kwenye eneo hili kuzaliana kwa wingi. Mabwawa na mito iliyopo katika hifadhi hii yanakuwa ndio sehemu nzuri zaidi ya kuona ndege wengi sana. Vile vile uoto wa asili katika hifadhi hii ndio unaopelekea wingi wa ndege katika eneo hili.

Ubao ulio katika njia panda karibu na Minjingu katika barabara ya Arusha-Dodoma ikikualika kutembelea Tarangire

Familia  nzima ya watalii ikipumzika na kupata mlo wa mchana eneo lijulikanalo kama Matete Picnic area katikati ya Tarangire
Watalii wakiangalia tembo wakinywa maji ya Mto Tarangire
Watalii wakiangalia wanyama eneo la Matete Picnic area.



Hivyo makala TEMBO, NDEGE, CHATU NA UBUYU WAVUTIA MAELFU YA WATALII KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE

yaani makala yote TEMBO, NDEGE, CHATU NA UBUYU WAVUTIA MAELFU YA WATALII KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TEMBO, NDEGE, CHATU NA UBUYU WAVUTIA MAELFU YA WATALII KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/tembo-ndege-chatu-na-ubuyu-wavutia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TEMBO, NDEGE, CHATU NA UBUYU WAVUTIA MAELFU YA WATALII KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE"

Post a Comment