title : DC Ilala mgeni rasmi kwenye kongamano la Changamka Mwanamke
kiungo : DC Ilala mgeni rasmi kwenye kongamano la Changamka Mwanamke
DC Ilala mgeni rasmi kwenye kongamano la Changamka Mwanamke
Mwambawahabari
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akisalimiana na Mkurugenzi WA Taasisi ya Changamka Mwanamke MARIA LUCAS Dar es Salam kwa ajili ya maandalizi ya semina ya Wanawake Wajasiliamali julai 21 NNSF ILALA (PICHA NA HERI SHAABAN)
Na Heri Shaban
MKUU wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema julai 21 mwaka huu anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kongamano la semina ya Changamka Mwanamke .
Semina imeandaliwa na taasisi ya Changamka Mwanamke yenye lengo la kuwajengea uwezo Wanawake wa Taasisi hiyo katika kazi za ujasiriamali .
Akizungumza na Waandishi wa Habari Dar es Salam jana Mkurugenzi wa Taasisi hiyo yenye makazi wilayani Ilala Maria Lucas alisema mafunzo hayo yatawashirikisha Wanachama wa Changamka Mwanamke na Wajasiriamali wa wanawake wa WILAYA ya Ilala na walio na biashara na wasio na biashara kutoka kata za Manispaa ya Ilala zote.
"Tumeandaa kongamano kubwa LA kuwakomboa Wanawake Wajasiriamali ,Changamka Mwanamke kwa ajili ya kuwajengea weledi waweze kupata Elimu itakayowafungulia mwanga katika utekekezaji wa majukumu yao na mgeni rasmi mkuu wa WILAYA wilaya ya Ilala Sophia Mjema "alisema Lucas.
Lucas alisema katika mafunzo Pia mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema atazindua harambee ya kutunisha mfuko wa mradi wa kilimo cha pilipili.
Alisema mafunzo hayo yatafanyika katika ukumbi wa NSSF ILALA Boma mkuu wa wilaya ya Ilala ataongozana na wageni waalikwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Angelina Malembeka na Makamu wa Rais wa Vicoba Tanzania Scholastika KEVELA.
Aidha alisema taasisi ya Changamka Mwanamke ilianzishwa mwaka 2016
Alisema Changamka Mwanamke inafanya shughuli zake mkoa Dar es Salam inashirikiana na Serikali katika shughuli mbali mbali za kijamii kabla kuanzisha taasisi hiyo amegundua Wanawake wana ndoto za kujikomboa kiuchumi lakini wanashindwa kutimiza ndoto zao kutokana na mazingira ya malezi pamoja na mfumo.
"Kutokana na fikra hizi Changamka Mwanamke imeweza kutambua hilo imekuwa ikitoa elimu mbalimbali kwa Wanawake ili kuweza kutimiza ndoto zao kuacha kuota tena kauli Mbiu Mwanamke jikomboe "alisema.
Hivyo makala DC Ilala mgeni rasmi kwenye kongamano la Changamka Mwanamke
yaani makala yote DC Ilala mgeni rasmi kwenye kongamano la Changamka Mwanamke Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC Ilala mgeni rasmi kwenye kongamano la Changamka Mwanamke mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/dc-ilala-mgeni-rasmi-kwenye-kongamano.html
0 Response to "DC Ilala mgeni rasmi kwenye kongamano la Changamka Mwanamke"
Post a Comment