title : WAZIRI UMMY ASHTUSHWA NA MSONGAMANO WA WAGONJWA TEMEKE
kiungo : WAZIRI UMMY ASHTUSHWA NA MSONGAMANO WA WAGONJWA TEMEKE
WAZIRI UMMY ASHTUSHWA NA MSONGAMANO WA WAGONJWA TEMEKE
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
Waziri wa Afya Wanawake,Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameshtushwa na wingi wa wagonjwa waliopo katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke na kuagiza katibu Mkuu wa Wizara hiyo kufanya utaratibu wa kuongeza madaktari ili kutoa huduma kwa ufanisi.
Waziri Ummy ametoa maagizo hayo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kutembelea Hospitali zote za Mikoa za Rufaa ambazo Rais Magufuli ameagiza zianze kuhudumiwa na Wizara ya afaya badala ya halmashauri husika.
"Nimetembelea hapa nimejionea mwenyewe kuwa na msongamano mkubwa sana hapa kiasi cha Daktari mmoja kuweza kuhudumia wagonjwa 300 kwa siku kwa mujibu wa maelezo ya Mganga mkuu wa hospitali hii jambo ambalo linahitaji kushughulikiwa mapema hivyo namuagiza katibu mkuu kuweza kuongeza madaktari hapa hili waweze kuwahudumia Wananchi kwa wakati"amesema Ummy.
Waziri Ummy pia alimwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kuhakikisha kuwa anaweka X Ray katika hospitali zilizopo chini yake hili kuweza kupunguza wimbi lka wagonjwa wengi amabo ukimbilia katika Hospitali hiyo.
Waziri wa Afya Wanawake Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na Mmoja wa Wanawake waliojifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke na kubaini kuwepo kwa idadi kubw aya wagonjwa kuliko kawaida kutokana na Daktari mmoja kihudumia wagonjwa zaidi ya 300 katika OPD.
Waziri wa Afya Wanawake Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizunguma na watu waliojaa katika Mapokezi ya Hospitali ya Rufaa Temeke amabo wanahudumiwa na madkatari wachache.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke, Dk Amani Malima akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya Wanawake Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kwanini hospitali hiyo ina wagonjwa wengi .
Sehemu ya Umati wa Wagonjwa waliofurika katika Hospitali ya Rufaa Temeke.
Waziri wa Afya Wanawake Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa Habari.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke Dr. Amani Malima akizungumza na Waandishi wa Habari.
Hivyo makala WAZIRI UMMY ASHTUSHWA NA MSONGAMANO WA WAGONJWA TEMEKE
yaani makala yote WAZIRI UMMY ASHTUSHWA NA MSONGAMANO WA WAGONJWA TEMEKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI UMMY ASHTUSHWA NA MSONGAMANO WA WAGONJWA TEMEKE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/waziri-ummy-ashtushwa-na-msongamano-wa.html
0 Response to "WAZIRI UMMY ASHTUSHWA NA MSONGAMANO WA WAGONJWA TEMEKE"
Post a Comment