Serikali kuwaenzi Wanamichezo Wakongwe

Serikali kuwaenzi Wanamichezo Wakongwe - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Serikali kuwaenzi Wanamichezo Wakongwe, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Serikali kuwaenzi Wanamichezo Wakongwe
kiungo : Serikali kuwaenzi Wanamichezo Wakongwe

soma pia


Serikali kuwaenzi Wanamichezo Wakongwe


Na Lorietha Laurence-WHUSM,Mbulu Mjini

Serikali imeandaa mpango wa kuwaenzi watu mashughuri wakiemo wanamichezo wakongwe ambao wamewahi kuliletea taifa heshima katika mashindano mbalimbali akiwemo mwanariadha Mkongwe Bw. John Steven Akwhari.

Hayo yamesemwa leo Mbulu Mjini na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza alipomtembelea mwanariadha huyo nyumbani kwake ambapo alipata fursa ya kuona medani , tuzo na vikombe alivyowahi kushinda mwanariadha huyo.

“ Sisi kama Wizara tumeanzisha kampeni ya Uzalendo ambapo mwaka jana tuliwaenzi wasanii wa zamani wa muziki na mwaka huu mnamo Oktoba 14 ni zamu ya wanamichezo wakongwe akiwemo Bw. John Akwhari ” amesema Mhe. Shonza .Alizidi kueleza kuwa amevutiwa na jinsi mwanariadha huyo anavyotunza kumbukumbu zake huku akiwataka wanamichezo na watu wengine kuiga mfano huo bora ili kuviwezesha vizazi vijavyo kupata historia nzuri katika sekta ya michezo.

Naye Mwanariadha Mkongwe Bw. John Steven Akwhari amesema amefurahi kuona Serikali inatambua na kuthamini mchango wake katika sekta ya michezo na kuhaadi kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili kwa pamoja kuleta maendeleo katika sekkta hiyo muhimu. 
 
 Bw. John Akwhari ni mwanariadha wa zamani wa Tanzania wa kwanza kufungua milango ya kushiriki riadha nje ya nchi ambapo alijizolea umaarufu katika mashindano ya mwaka 1968 ya Olimpiki nchini Mexico ambapo licha ya kuwa wa mwisho aliueleza umati kuwa nchi yake ilimtuma kumaliza mbio na siyo kuanza mbio.
 Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (Kushoto)  akiangalia vikombe vya ushindi alivyowahi kushinda Mwanariadha Mkongwe Bw. John Akwhari (Kulia) alipofanya ziara ya kutembelea nyumbani kwake Mjini Mbulu hapo Jana.


 


Hivyo makala Serikali kuwaenzi Wanamichezo Wakongwe

yaani makala yote Serikali kuwaenzi Wanamichezo Wakongwe Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Serikali kuwaenzi Wanamichezo Wakongwe mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/serikali-kuwaenzi-wanamichezo-wakongwe.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Serikali kuwaenzi Wanamichezo Wakongwe"

Post a Comment