title : Naibu Waziri Shonza atoa wito Kwa Halmashauri kutenga Fedha kuboresha miundo mbinu ya michezo.
kiungo : Naibu Waziri Shonza atoa wito Kwa Halmashauri kutenga Fedha kuboresha miundo mbinu ya michezo.
Naibu Waziri Shonza atoa wito Kwa Halmashauri kutenga Fedha kuboresha miundo mbinu ya michezo.
Na Lorietha Laurence-WHUSM, Mbulu
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ametoa wito kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mjini kuhakikisha wanatengeneza miundo mbinu ya michezo hususani viwanja vya michezo.
Akizungumza wakati wa fainali za kombe la Issay lililoandaliwa na Mbunge wa Mbulu Mjini Mhe. Zacharia Isaay jana mjini hapo , lengo ikiwa ni kutoa hamasa ya michezo kwa wakazi wa eneo hilo. “Ni jukumu la viongozi wa Halmashauri kuhakikisha kuwa kila mwaka wanatenga fedha katika bajeti zao ambazo zitasaidia katika kuboresha miundo mbinu ya michezo ” amesema Mhe. Juliana Shonza.
Anazidi kueleza kuwa michezo ni muhimu sana kwa jamii,mbali na kuwaleta watu pamoja imekuwa ni chanzo kizuri cha ajira kwa vijana na hivyo kuwasaidia katika kukuza uchumi wao binafsi. idha Mhe. Juliana Shonza amempongeza Mbunge wa Mbulu Mjini Mhe.Zacharia Isaay kwa kuhamasisha michezo na juhudi alizozionyesha katika kufanikisha mashindano hayo na kuwaomba wadau na wananchi wengine kuunga mkono juhudi hizo.
Vilevile aliwataka Maafisa Michezo kuhakikisha wanaweka mikakati mbalimbali ya kuhimiza michezo mashuleni ili kuweka hamasa kwa wanafunzi kupenda na kujihusisha na michezo. wa upande wake Mbunge wa Mbulu Mjini Mhe. Zacharia Isaay alimshukuru mgeni rasmi kwa kuweza kufunga mashindano hayo na kuaahidi kuendelea kutoa hamasa ya michezo kwa wananchi wa Halmashauri ya Mbulu Mji na Vitongoji vyake.
Mashindano ya Isaay Cup yalianza tarehe 15 mwezi wa tano na kumalizika tarehe 20 ya mwezi wa sita kwa ngazi ya Tarafa, na baadaye kuingia katika ngazi ya Jimbo kuanzia tarehe 21 mwezi wa sita mwaka huu huku yakishirikisha jumla ya michezo 26 ikiwemo riadha, mpira wa miguu, mpira wa nyavu na netball .
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akiongea wakati wa kufunga mashindano ya Kombe la Isaay lililoandaliwa na Mbunge wa Mbulu Mjini Mhe. Zacharia Isaay lengo ikiwa ni kutoa hamasa ya michezo kwa wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu pamoja na vitongoji vyake.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akimkabidhi zawadi mshindi wa mbio za kilomita 10 kwa upande wa wanawake Bibi. Olivia Alfred wakati wa kufunga mashindano ya kombe la Isaay kulia ni Mbunge wa Mbulu mjini aliyeandaa mashindano hayo Mhe. Zacharia Isaay na kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu Bibi.Sarah Sanga.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akikabidhi kombe kwa timu ya mpira wa miguu ya Bodaboda Fc ambao waliibuka washindi dhidi ya wapinzani wao Home Boys Fc wakati wa fainali za kombe la Isaay lililoandaliwa na Mbunge wa Mbulu Mjini Mhe. Zacharia Isaay hapo jana.

Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (mwenye kipaza sauti ) akitoa nasaha kwa timu zizizoingia fainali ambazo ni Home Boys na Bodaboda Fc kabla ya mechi ya kutamfuta mshindi wa kwanza katika mashindano ya kombe la Issay lililoandaliwa na Mbunge wa Mbulu Mjini Mhe. Zacharia Isaay jana mjini hapo.
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisalimiana na wachezaji wa kike wa mpira wa miguu kutoka shule ya Sekondari ya Chief Sarwatt ambao waliibuka washindi dhidi ya shule ya Sekondari ya Nowu wakati wa fainali ya Kombe la Isaay lililoandaliwa na Mbunge wa Mbulu Mjini Mhe.Zacharia Isaay hapo jana .
(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,MBULU MJINI).
Hivyo makala Naibu Waziri Shonza atoa wito Kwa Halmashauri kutenga Fedha kuboresha miundo mbinu ya michezo.
yaani makala yote Naibu Waziri Shonza atoa wito Kwa Halmashauri kutenga Fedha kuboresha miundo mbinu ya michezo. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Waziri Shonza atoa wito Kwa Halmashauri kutenga Fedha kuboresha miundo mbinu ya michezo. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/naibu-waziri-shonza-atoa-wito-kwa_4.html
0 Response to "Naibu Waziri Shonza atoa wito Kwa Halmashauri kutenga Fedha kuboresha miundo mbinu ya michezo."
Post a Comment