title : MWILI WA MAMA YAKE SHIGONGO WAAGWA DAR, KUZIKWA JUMATANO JIJINI MWANZA
kiungo : MWILI WA MAMA YAKE SHIGONGO WAAGWA DAR, KUZIKWA JUMATANO JIJINI MWANZA
MWILI WA MAMA YAKE SHIGONGO WAAGWA DAR, KUZIKWA JUMATANO JIJINI MWANZA
Na Leandra Gabriel, Blogu wa jamii
MWILI wa Mama mzazi wa Mkurugenzi wa Makampuni ya Global Group, Mtunzi na mjasiriamali Eric Shigongo umeagwa leo katika kanisa katoliki la Mtakatifu Martha Mikocheni B jijini Dar es salaam na jioni ya leo utapelekwa katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere kwa ajili ya kusafirishwa kuelekea Jijini Mwanza katika kijiji cha Bupandwahela kwa maziko.
Imeelezwa kwamba mwili wa Bi. Asteria utapokelewa Nyakato Mwanza siku ya Jumatatu asubuhi na kuagwa majira ya saa kumi jioni na siku ya jumanne safari ya kuelekea Bupandwamhela kwa maziko itaanza.
Bi. Asteria atapumzishwa katika makao yake ya milele siku ya jumatano, Agosti 1 mwaka huu.
Marehemu alizaliwa Septemba 16, 1931 akiwa mtoto wa 3 kati ya watoto 3 kwa mama Asteria ambaye alifariki mara baada ya kujifungua mtoto wake wa mwisho ambaye ni mama wa Eric Shigongo na nduguze, marehemu alikuwa mjasiriamali na alibahatika kupata watoto 11 na walio hai ni 9 pekee, na ameacha wajukuu 42 na vitukuu 23.
Bi Asteria alianza kuugua muda mrefu akisumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu na kupata matibabu katika hospitali mbalimbali kama vile TMJ, Agha khan na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambako mauti yalimfika Julai 27 mwaka huu.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake Lihimidiwe. Amina.
Eric Shigongo akisoma wasifu wa marehemu mama yake Wakati wa kuaga
Pichani wa Nne kushoto,Ndugu Eric shigongo akiwa na baadhi ya Ndugu jamaa na marafiki wakati wa kuaga mwili ya Mama yake mzazi nyumbani kwake Mikocheni B,Kinondoni jijini Dar
Hivyo makala MWILI WA MAMA YAKE SHIGONGO WAAGWA DAR, KUZIKWA JUMATANO JIJINI MWANZA
yaani makala yote MWILI WA MAMA YAKE SHIGONGO WAAGWA DAR, KUZIKWA JUMATANO JIJINI MWANZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MWILI WA MAMA YAKE SHIGONGO WAAGWA DAR, KUZIKWA JUMATANO JIJINI MWANZA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/mwili-wa-mama-yake-shigongo-waagwa-dar.html
0 Response to "MWILI WA MAMA YAKE SHIGONGO WAAGWA DAR, KUZIKWA JUMATANO JIJINI MWANZA"
Post a Comment