title : Mawaziri watano wajadili Bomba la Mafuta
kiungo : Mawaziri watano wajadili Bomba la Mafuta
Mawaziri watano wajadili Bomba la Mafuta
Mawaziri kutoka Wizara Tano zinazohusika na utekelezaji wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanzania, wamekutana na wataalam wa Tanzania walio katika Timu ya Kitaifa ya Majadiliano ya mradi ili kupata taarifa ya utekelezaji wa mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwaka 2020.
Kikao hicho kilichoongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kimefanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dodoma ambapo Mawaziri waliohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji.
Viongozi wengine waliohudhuria ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari, Mhandisi Karim Mataka na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),Mhandisi Kapuulya Musomba.
Pamoja na kupata taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Bomba la Mafuta kutoka katika Timu hiyo ya Taifa ya Majadiliano (GNT), Mawaziri hao pamoja na wataalam mbalimbali walijadili changamoto mbalimbali pamoja na utatuzi wake lengo likiwa ni kutekeleza mradi huo kwa ufanisi ndani ya muda uliopangwa.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( wa Nne kulia), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (wa Tatu kushoto), Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (wa Tatu kulia), Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde (wa kwanza kulia) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (wa Pili kulia) wakiwa katika kikao kilichokuwa kikijadili mradi wa Bomba la Mafuta jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( katikati), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (kulia kwa Waziri wa Nishati), Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (kushoto kwa Waziri wa Nishati), Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde (haonekani pichani) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (haonekani pichani) wakiwa katika kikao kilichokuwa kikijadili mradi wa Bomba la Mafuta jijini Dodoma. Wengine ni Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi mbalimbali za Serikali.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Mawaziri watano wajadili Bomba la Mafuta
yaani makala yote Mawaziri watano wajadili Bomba la Mafuta Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mawaziri watano wajadili Bomba la Mafuta mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/mawaziri-watano-wajadili-bomba-la-mafuta.html
0 Response to "Mawaziri watano wajadili Bomba la Mafuta"
Post a Comment