title : WAZIRI MKUU AZINDUA FAO LA USHIRIKA AFYA LA NHIF
kiungo : WAZIRI MKUU AZINDUA FAO LA USHIRIKA AFYA LA NHIF
WAZIRI MKUU AZINDUA FAO LA USHIRIKA AFYA LA NHIF
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua fao la Ushirika Afya ambalo linawalenga wananchi wanaojishughulisha na kilimo kupitia ushirika.
Amezindua fao hilo jana (Jumatatu, Julai 16, 2018) kwenye mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ulowa katika kijiji cha Kangeme, kata ya Ulowa, Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, Shinyanga.
Waziri Mkuu alikabidhi kadi 20 kwa niaba ya wanachama 259 ambao wamejiunga na mpango huo. Wanachama hao wanatoka katika vyama mbalimbali vya ushirika kwenye Halmashauri ya Ushetu, wilayani Kahama.
Amesema katika kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata huduma za afya katika hospitali yoyote ile nchini, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, wameamua kuzindua mpango wa Ushirika Afya, ambao unahusisha wakulima walio katika vyama vya ushirika.
“Gharama ya kujiunga na fao hili kwa mwaka ni sh. 76,000 kwa mtu mmoja na sh. 50,400 kwa mtoto mmoja lakini unakuwa na uhakika wa kutibiwa katika hospitali yoyote ile hapa nchini,” amesema.
Amesema takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa Tanzania kuna vyama vya ushirika 10,522 vyenye wanachama 2,234,000 ambapo asilimia 35 ya wanaushirika huwa wanapata magonjwa ya dharura na wanakuwa hawana namna ya kupata fedha kwa haraka.
“Tunatambua wote kuwa fedha ya mkulima ni ya msimu, lakini mkulima ukiwa na kadi ya bima ya afya, utapata matibabu kokote kule hata kama huna fedha taslimu,” amesema.Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumpongeza kijana aliyebuni mpango huo ambaye anatoka Taasisi ya Ukuzaji wa Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), Mwombeki Baregu.
“Huyu kijana si mwajiriwa wa NHIF, wala siyo mtumishi Serikalini, lakini kwa sababu ya uzalendo, alikuja na huu mfumo akauelezea na kuonesha manufaa yake kwa wananchi wa kawaida, na kwa sababu Serikali yenu ni sikivu, tukaufanyia kazi na leo ninauzindua,” amesema.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi kadi ya bima ya afya mmoja wa wakulima waliopo kwenye Ushirika huo ambapo wanachama 120 wamepatiwa kadi hizo na wanachama 200 wameshajaza fomu za kijiunga
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe mfano wa kadi ya bima ya afya kwa matibabu kwa vyama vya Ushirika wilayani Ushetu
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa akimkabidhi kadi ya bima ya afya ya Ushirika Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bernad Konga akizungumzia Fao hilo ambalo litawanufaisha wakulima wa mazao waliopo kwenye vyama vya msingi.
Hivyo makala WAZIRI MKUU AZINDUA FAO LA USHIRIKA AFYA LA NHIF
yaani makala yote WAZIRI MKUU AZINDUA FAO LA USHIRIKA AFYA LA NHIF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AZINDUA FAO LA USHIRIKA AFYA LA NHIF mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/waziri-mkuu-azindua-fao-la-ushirika.html
0 Response to "WAZIRI MKUU AZINDUA FAO LA USHIRIKA AFYA LA NHIF"
Post a Comment