title : Kesi ya Sethi na Rugemalira yazidi kupigwa Kalenda
kiungo : Kesi ya Sethi na Rugemalira yazidi kupigwa Kalenda
Kesi ya Sethi na Rugemalira yazidi kupigwa Kalenda
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mara nyingine tena, imeipiga kalenda kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili, Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habinder Seth na mwenzake James Rugemalira imeahirishwa hadi Julai 19/2018 sababu upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Wakili Serikali Mwandamizi, Mtalemwa Kishenyi akisaidiana na wakili kutoka Takukuru, Leonard Swai, alidai mahakamani hapo kuwa, kesi hiyo leo imekuja kwa kutajwa na kuiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo kwani upelelezi bado haijakamilika.
Alidai kuwa wapo kati hatua za mwisho kukamilisha upelelezi.
Kufuatia maelezo hayo, wakili wa utetezi, Hajra Mungula akisaidia na Dora Malaba, waliutaka upande wa mashtaka kuhakikisha upelelezi unakamilika kwa wakati, ili kesi iweze kuendelea.
Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi, anayesikiliza kesi hiyo, ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 19, 2018.
Sethi na Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kughushi, kutoa nyaraka za kughushi.
Pia wanadaiwa kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Hivyo makala Kesi ya Sethi na Rugemalira yazidi kupigwa Kalenda
yaani makala yote Kesi ya Sethi na Rugemalira yazidi kupigwa Kalenda Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kesi ya Sethi na Rugemalira yazidi kupigwa Kalenda mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/kesi-ya-sethi-na-rugemalira-yazidi.html
0 Response to "Kesi ya Sethi na Rugemalira yazidi kupigwa Kalenda"
Post a Comment