SERIKALI YATOA SHILINGI BILIONI 24.4 KUJENGA NA KUKARABATI MELI

SERIKALI YATOA SHILINGI BILIONI 24.4 KUJENGA NA KUKARABATI MELI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YATOA SHILINGI BILIONI 24.4 KUJENGA NA KUKARABATI MELI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YATOA SHILINGI BILIONI 24.4 KUJENGA NA KUKARABATI MELI
kiungo : SERIKALI YATOA SHILINGI BILIONI 24.4 KUJENGA NA KUKARABATI MELI

soma pia


SERIKALI YATOA SHILINGI BILIONI 24.4 KUJENGA NA KUKARABATI MELI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa shilingi bilioni 24.496 kwa ajili ya kujenga meli mpya mbili na kukarabati meli tano ili ziweze kutoa huduma ya uchukuzi wa kusafirisha abiria na mizigo katika maziwa makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa. 

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu ujenzi wa meli katika maziwa makuu kwenye kikao kilichofanyika bungeni mjini Dodoma. 

Mhe. Nditiye aliongeza kuwa fedha hizo tayari zimeshatolewa na Serikali na kupatiwa Kampuni ya MSCL kwa ajili ya kuanza ujenzi wa meli 2 mpya za kubeba abiria na mizigo katika ziwa Tanganyika na Victoria na kukarabati meli 5 ambazo ni MV. Victoria, MV. Butiama, MV. Liemba, MV. Umoja na MV. Serengeti. 

Mhandisi Nditiye aliongeza kuwa lengo la Serikali la kutoa fedha hizo ni kuboresha huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo katika maziwa makuu ili wananchi waweze kupata huduma za usafiri wa uhakika; kwa wakati na zinazozingatia usalama wa abiria na mizigo yao; kuiwezesha Serikali kupata mapato na kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla; na kwa kutambua fursa ya biashara iliyopo kwenye maziwa hayo kwa kuzingatia kuwa meli hizo ni kiungo kikubwa baina ya nchi yetu na nchi za jirani za Uganda, Kenya, Zambia, Malawi na DRC Congo kwa kuwa zinatumia meli zetu kusafirisha abiria na mizigo yao kupitia maziwa hayo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akipata maelezo kutoka kwa Kapteni Desiderius Chuwa wa Meli ya MV. Clarias kuhusu usalama wa chombo hicho na abiria wake kabla ya kuanza safari ya kutoka Mwanza kwenda Kisiwa cha Ukerewe wakati wa ziara yake mkoani Mwanza.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa maelekezo kuhusu usalama wa abiria na matumizi ya vifaa vya uokoaji majini kwa watendaji na abiria wa meli ya MV. Clarias kabla ya kuanza safari ya kutoka Mwanza kwenda Kisiwa cha Ukerewe wakati wa ziara yake mkoani humo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akipatiwa maelezo kuhusu matengenezo ya yaliyofanyika ya mfumo wa mafuta wa meli ya MV. Clarias inayosafirisha abiria kutoka Mwanza kwenda Kisiwa cha Ukerewe wakati wa ziara yake mkoani humo. Wa kwanza kulia ni Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSL) Bwana Eric Hamissi.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) akikagua meli ya MV. Clarias inayosafirisha abiria kutoka Mwanza kwenda kisiwa cha Ukerewe wakati wa ziara yake mkoani humo. Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSL) Bwana Eric Hamissi (kushoto) akitoa maelezo kuhusu meli hiyo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) alipokagua meli ya MV. Clarias inayomilikiwa na Kampuni ya Huduma za Meli (MSL) ikiwa tayari kusafirisha abiria kutoka Mwanza kwenda kisiwa cha Ukerewe wakati wa ziara yake mkoani humo. 



Hivyo makala SERIKALI YATOA SHILINGI BILIONI 24.4 KUJENGA NA KUKARABATI MELI

yaani makala yote SERIKALI YATOA SHILINGI BILIONI 24.4 KUJENGA NA KUKARABATI MELI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YATOA SHILINGI BILIONI 24.4 KUJENGA NA KUKARABATI MELI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/serikali-yatoa-shilingi-bilioni-244.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI YATOA SHILINGI BILIONI 24.4 KUJENGA NA KUKARABATI MELI"

Post a Comment