JAFO AWAPONGEZA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA

JAFO AWAPONGEZA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JAFO AWAPONGEZA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JAFO AWAPONGEZA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA
kiungo : JAFO AWAPONGEZA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA

soma pia


JAFO AWAPONGEZA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewapongeza wanafunzi na walimu wa Shule ya sekondari Kibaha kwa kushika nafasi ya kwanza Kitaifa kwenye matokeo ya kidato sita mwaka huu yaliyotangazwa mwishoni mwa wiki. 

Jafo ametoa pongezi hizo leo katika shule hiyo ambayo ni miongoni mwa shule alizozitembelea Januari mwaka huu na kuweka mikakati ya kuhamasisha shule hizo zifanye vyema kwenye mitihani ya Kitaifa.

Waziri Jafo amesisitiza kwamba matokeo haya mazuri yanayoanza kujitokeza kwa shule za serikali yametokana na juhudi kubwa ya Rais John Magufuli katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ambapo shule kongwe zote zipo katika hatua mbalimbali ya ukarabati sambamba na maboresho mengine katika sekta ya elimu. 

Jafo amemshukuru Rais Magufuli kwa moyo wake wa kuipambania jamii ya watanzania hadi kufikia mafanikio hayo makubwa yanayoanza kujitokeza hapa nchini. 

Aidha Jafo ameanza mkakati wa kuzifanya shule za serikali hapa nchini kushika nafasi zaidi ya sita katika ya kumi bora kwa matokeo ya kidato cha sita mwakani. Katika kufanikisha mkakati huo, Waziri Jafo ameitisha kikao cha kazi kwa wakuu wa shule pamoja na walimu wa taaluma wa shule za sekondari za vipaji maalum na shule za serikali zilizoingia katika nafasi ya 30 bora katika matokeo ya kidato cha sita ya mwaka huu ambapo kikao hicho kinatarajiwa kufanyika jijini Dodoma Agosti 2 mwaka huu.

Awali, kabla ya pongezi hizo,Walimu na wanafunzi wa Kibaha wamekiri wazi kwamba hamasa aliyotoa Waziri Jafo iliwafanya kuwa na uchungu na nguvu ya mapambano katika elimu hadi kufikia mafaniko hayo makubwa waliyoyapata.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akizungumza na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibaha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akipokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha.
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Kibaha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akikagua ukarabati wa miundombinu katika shule ya sekondari Kibaha.


Hivyo makala JAFO AWAPONGEZA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA

yaani makala yote JAFO AWAPONGEZA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JAFO AWAPONGEZA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/jafo-awapongeza-shule-ya-sekondari.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "JAFO AWAPONGEZA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA"

Post a Comment