Matonya naye ataka kwenda kuonana na Rais Magufuli Kumshukuru kwa Msamaha

Matonya naye ataka kwenda kuonana na Rais Magufuli Kumshukuru kwa Msamaha - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Matonya naye ataka kwenda kuonana na Rais Magufuli Kumshukuru kwa Msamaha, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Matonya naye ataka kwenda kuonana na Rais Magufuli Kumshukuru kwa Msamaha
kiungo : Matonya naye ataka kwenda kuonana na Rais Magufuli Kumshukuru kwa Msamaha

soma pia


Matonya naye ataka kwenda kuonana na Rais Magufuli Kumshukuru kwa Msamaha

Wakati Babu Seya na mwanaye wakiwa tayari wametimiza azima yao ya kumuona Rais, Mganga Matonya, aliyeepushwa kifungo cha maisha, analalamikia hali yake kuwa imemzuia kusafiri kwenda Ikulu kumueleza jambo Rais John Magufuli.

Matonya, ambaye alikuwa mfungwa mwenye umri mkubwa kuliko wote kati ya walioachiwa huru, alikuwa anatumikia kifungo cha maisha baada ya awali kupata msamaha wa adhabu ya kunyongwa kutokana na kupatikana na hatia ya kuua na ameishi gerezani miaka 43.

“Mtakumbuka nilikuwa mtu wa kwanza kati ya tuliotoka gerezani niliyetamka kutaka nimuone Rais, lakini hadi sasa nashindwa kumuona,” alisema Matonya ambaye  siku alipotoka Gerezani alisema ana neno la kumueleza Rais na asipopata nafasi, atakufa nalo.

“Siko tayari kumwambia mtu mwingine zaidi ya Magufuli kipenzi changu,” alisema.

Akizungumza kwa simu kutoka Kijiji cha Wiliko, Matonya alisema taarifa za wanamuziki hao alizipata kutoka kwa mtoto wake na kwamba zilimliza kwani angepata nafasi hiyo kabla hajafa, angejisikia huru katika nafsi yake.

“Alipokuja (Rais Magufuli) kwenye mkutano wa CCM Dodoma niliwaomba watoto wangu wanipeleke. Tatizo wanaona kama nimechanganyikiwa lakini siyo kweli,” alisema Matonya.

Mzee huyo aliomba taasisi na mashirika mengine kumsaidia kumuona Rais Magufuli.

Mtoto wake, Aron alisema aandike ujumbe wake hata magazetini na Rais atauona.


Hivyo makala Matonya naye ataka kwenda kuonana na Rais Magufuli Kumshukuru kwa Msamaha

yaani makala yote Matonya naye ataka kwenda kuonana na Rais Magufuli Kumshukuru kwa Msamaha Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Matonya naye ataka kwenda kuonana na Rais Magufuli Kumshukuru kwa Msamaha mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/matonya-naye-ataka-kwenda-kuonana-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Matonya naye ataka kwenda kuonana na Rais Magufuli Kumshukuru kwa Msamaha"

Post a Comment