title : AWESO AMURU KUWEKWA NDANI WAKANDARASI WA MRADI WA MAJI HANDENI KWA KUSHINDWA KUWEPO ENEO LA MRADI
kiungo : AWESO AMURU KUWEKWA NDANI WAKANDARASI WA MRADI WA MAJI HANDENI KWA KUSHINDWA KUWEPO ENEO LA MRADI
AWESO AMURU KUWEKWA NDANI WAKANDARASI WA MRADI WA MAJI HANDENI KWA KUSHINDWA KUWEPO ENEO LA MRADI
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ameamuru kuwekwa ndani wakandarasi wanaotekelezwa mradi wa maji yenye thamani ya zaidi ya bilioni tatu eneo la mkata wilayani Handeni baada ya kushindwa kuwepo kwenye eneo la mradi licha ya kupewa taarifa za uwepo wa ziara yake.
Wakandarasi ambao walilazimika kuwekwa ndani ni Mkandarasi wa Kampuni ya Tansino Logistick Limited ya Dar Abdul Ismail na Charles Stephano ambaye ni mkandarasi wa ujenzi huku Chales Tarimbo mshauri Mkandarasi naye akikumbana na kadhia hiyo.
Agizo hilo alilitoa leo wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maji inayotekelezwa kwenye kata ya Mkata wilayani Handeni ambapo miradi hiyo mitatu ilikuwa ikigharimu zaidi ya sh.bilioni tatu.
Akiwa kwenye eneo hilo Naibu Waziri huyo alisema haiwezekani wabunge wanaomba miradi ya maji na serikali inatenga lakini watu wachache wanatumia fedha hizo kwenye matumizi kwa maslahi yao binafasi na kuwafanya wananchi kuendelea kuteseka na tatizo la maji.
Alisema kutokana na kuwepo kwa tabia hiyo ambayo imekuwa ikirudisha nyuma juhudi kubwa zinazofanywa serikali hawatavumiliwa badala yake watahakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuweza kukomesha vitendo vya namna hiyo kwenye jamii.
Hivyo makala AWESO AMURU KUWEKWA NDANI WAKANDARASI WA MRADI WA MAJI HANDENI KWA KUSHINDWA KUWEPO ENEO LA MRADI
yaani makala yote AWESO AMURU KUWEKWA NDANI WAKANDARASI WA MRADI WA MAJI HANDENI KWA KUSHINDWA KUWEPO ENEO LA MRADI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AWESO AMURU KUWEKWA NDANI WAKANDARASI WA MRADI WA MAJI HANDENI KWA KUSHINDWA KUWEPO ENEO LA MRADI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/aweso-amuru-kuwekwa-ndani-wakandarasi.html
0 Response to "AWESO AMURU KUWEKWA NDANI WAKANDARASI WA MRADI WA MAJI HANDENI KWA KUSHINDWA KUWEPO ENEO LA MRADI"
Post a Comment