title : KATIBU MKUU IKULU DKT.KUSILUKA AKUTANA NA UONGOZI WA TASAF
kiungo : KATIBU MKUU IKULU DKT.KUSILUKA AKUTANA NA UONGOZI WA TASAF
KATIBU MKUU IKULU DKT.KUSILUKA AKUTANA NA UONGOZI WA TASAF
Na Estom Sanga-TASAF
Katibu Mkuu mpya wa Ofisi ya Rais Dr Moses Kusiluka ametembelea ofisi za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF jijini Dar es salaam hii ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu ateuliwa na Rais John Magufuli kushika wadhifa huo mwezi uliopita.
Akizungumza na Menejimenti ya TASAF ,Dr. Kusiluka amesema ziara hiyo imelenga kupata maelezo ya shughuli za Mfuko huo ambao uko chini ya Ofisi ya Rais. Aidha Katibu Mkuu huyo wa Ofisi ya Rais ameitaka menejimenti ya TASAF kuendelea kutoa huduma zake kwa umma kwa kuzingatia misingi ya uadilifu kama ambavyo serikali ya Awamu ya Tano inavyosisitiza.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TASAF,Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo Bw. Ladislaus Mwamanga amesema tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo mwaka 1999/2000 umefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hususani katika sekta za elimu, afya,miundombinu na uzalishaji mali katika maeneo mbalimbali nchini. “tumeshirikiana na wananchi katika kutatua kero na changamoto kwenye maeneo yao kwa mafanikio makubwa” amesema Bw. Mwamanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF pia amemweleza Katibu Mkuu huyo wa Ofisi ya Rais hatua mbalimbali zilizofikiwa na Mfuko katika kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao mkazo wake ni kuwawezesha walengwa kufanya kazi na kujipatia kipato kitakachowawezesha kuondokana na umaskini.
Bw. Mwamanga amesema tathimini ya awali inaonyesha kuwa mafanikio makubwa yamepatikana kwa Walengwa kuanza kuboresha maisha yao ikiwemo kujenga nyumba bora,kuboresha lishe ,elimu,kuwekeza katika miradi midogo midogo ikiwemo ufugaji wa kuku,mbuzi,nguruwe na hata ng’ombe na hivyo kujiongezea kipato chao.
Kuhusu huduma za kijamii Mkurugenzi mtendaji huyo wa TASAF amesema taasisi hiyo imeendelea kutoa mchango wa ujenzi wa visima vya maji katika maeneo mbalimbali nchini kwa kuwashirikisha wananchi kwenye maeneo yao. Dr. Moses Kusiluka ameteuliwa na Rais John Magufuli kushika wadhifa wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na kabla ya hapo alikuwa Katika Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Mkazi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Dr. Moses Kusiluka (kulia ) akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga (kushoto) katika maeneo ya Ofisi za TASAF jijini Dar es Salaam.
Dkt.r. Kusiluka akiwa katika jengo la mikutano la TASAF akiangalia ofisi zinazotumiwa na baadhi ya watumishi wa taasisi hiyo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Dr. Moses Kusiluka akizungumza na menejimenti ya TASAF alipotembelea taasisi hiyo kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na Rais John Magufuli kushika wadhifa huo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Moses Kusiluka (walioketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya TASAF baada ya kuzungumza nayo.
Hivyo makala KATIBU MKUU IKULU DKT.KUSILUKA AKUTANA NA UONGOZI WA TASAF
yaani makala yote KATIBU MKUU IKULU DKT.KUSILUKA AKUTANA NA UONGOZI WA TASAF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU MKUU IKULU DKT.KUSILUKA AKUTANA NA UONGOZI WA TASAF mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/katibu-mkuu-ikulu-dktkusiluka-akutana.html
0 Response to "KATIBU MKUU IKULU DKT.KUSILUKA AKUTANA NA UONGOZI WA TASAF"
Post a Comment