title : RAIS MAGUFULI APOKEA GAWIO LA TSH BILIONI 736 KUTOKA TAASISI ZA UMMA
kiungo : RAIS MAGUFULI APOKEA GAWIO LA TSH BILIONI 736 KUTOKA TAASISI ZA UMMA
RAIS MAGUFULI APOKEA GAWIO LA TSH BILIONI 736 KUTOKA TAASISI ZA UMMA

Mwamba wa habari
Kupatikana kwa jumla ya shilingi bilioni 736.36 kama gawio la mwaka wa fedha 2017/2018 kwa serikali kutoka makampuni,taasisi na mashirika ya umma 43 miongoni mwa zaidi ya 90 yanayojiendesha kibiashara, kiasi hicho kimetafsiriwa na serikali kama dalili za kuelekea kwenye mafanikio ya matarajio yake ya kuongeza pato la taifa toka mashirika hayo yalitobinafsishwa kwa wawekezaji.
Mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. John Magufuli, aliyekutana na wasimamizi na watendaji wakuu wa mashirika hayo jijini Dar es Salaaam leo, hata hivyo akillinganisha na mtaji wa

trilioni 49.05 na matarajio ya serikali ya gawio la asilimia 15 za mapato ghafi toka kila shirika linalotarajiwa kutoa gawio hilo amesisitiza ufanisi zaidi ili kufanikisha lengo la serikali.
Rais Magufuli ufuatiliaji wa serikali umegundua sababu kadhaa zinazosababisha mashirika mengi kushindwa kutoa gawio, yakiwemo udanganyifu, ubadhirifu, rushwa, uzembe na ukosekanaji wa ufuatiliaji makini kwa hayo mashirika. “watu walioaminiwa na kupewa mashirika wanaungana na wawekezaji kuiibia serikali” amefadhaishwa Rais Magufuli.
Rais amemwagiza Msajili wa Hazina, Doto James kuhakikisha kuwa mashirika yote yanayostahili kutoa gawio, yatoe gawio kinyume chake uongozi wake uondolewe, na kuwa hakuna haja ya kuendelea kukaa na shirika ambalo lipo tu bila kuwa na pesa.”Hapa pesa kwanza,” amesema Rais.

Makampuni mengine hapa nchini hufanya kazi kama kampuni tanzu na wanakuwa nakampuni zingine nchi za njekama mbinu za kuhamisha mali, kadhalkai, kuchukua mikopo nje ya nchi na uendeshaji unapangwa kuonyesha kuwa gharama ni kubwa na kusababisha hasara, amemwagiza Gavana wa Benki Kuu kuhakikisha kuwa kila mkopo anaochukua mwekezaji nje usajiliwe.
Rais alisema kuwa baadhi ya wawekezaji wanafanya udanganyifu huo kwa nia ya kutaka kuonyesha mahesabu ya hasara kila mwaka na matokeo yake ni kuikosesha serikali gawio lake, “kila siku makampuni yanasema yanapata hasara, si yafunge?’ alihoji Rais Magufuli.
Awali kabla ya kupokea mifano ya hundi za wawekezaji hao, Msajili wa Hazina Dotto James alimweleza Rais , wakuu wa mashirika hayo na wasimamizi wao wakiwemo mawaziri kadhaa matokeo ya tathmini ya amshirika hayo yaliyofanywa hivi karibuni na ofisi ya Msajili wa Hazina na Wizara ya Fedha na Mipango kuwa tathmini imeonesha kutoridhishwa na uendeshaji wa mashirika hilo.
Msajili wa Hazina amesema kuwa ubinafsishaji huo uliofanyika zaidi ya miaka 20 iliyopita tarajio la serikali lilikuwa ni kupanua miradi kwa kukuza mitaji na kuongeza mapato ya taifa na wigo wa ajira lakini mashirika mengi yamegeuka kuwa mzigo kwa serikali na hata kupewa ruzuku.
Zoezi la tathmini hiyo limepitia viwanda 85 vilivyobinafsishwa, wakati 51 vimefunga, 14 vina hali mbaya, na 20 vinazalisha vema, kadhalika vingine 12 mikataba ya mauzo na uwekezaji imeonekana kuwa na kasoro mbalimbali.
Kwa mazingira hayo, Msajili amesema wahusika wamepewa ilani ya wao kuwa tayari kufunga miradi yao ili kuirudisha serikalini tayari kupewa wawekezaji walio tayari kuzalisha kwa faida, lakini akatahadharisha kuwa zoezi hilo lisitafsiriwe kama kutaifisha, akasema lengo la serikali kuona kila mradi unazalisha kwa faida. Msajili amesema wawekezaji 9 mwezi huu mwanzoni wameamua kurudisha serikalini miradi yao.
Kwa upande wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma inayoongozwa na Mbunge Raphaeli Chegeni, imemhakikishia Rais Magufuli kuwa, imejipanga kuhakikisha kila mradi wa umma lazima uzalishe kwa faida na watendaji wote watakaoshindwa kuzalisha ama kusimamia nafasi zao wataondolewa, “Tumejipanga Mheshimiwa Rais, asiyeweza ni bora ajiondoe mwenyewe mapema kabla hatujamfikia,” amesema Mwenyekiti Chegeni.
Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango akimkaribisha mgeni rasmi Rais Magufuli kuongea na wahudhuriaji alisema mashirika yote kila Mtendaji Mkuu ameagizwa kuja na Mpango Kazi mpya utakaoonyesha shirika lake kuweza kuzalisha kwa faid a ya kufanikisha gawio la serikali, akaonya kuwa pamoja na kuwepo changamoto kila Mtendaji akipambana na mapungufu ya uzembe, ubadhirifu malengo yatafanikishwa.
Hivyo makala RAIS MAGUFULI APOKEA GAWIO LA TSH BILIONI 736 KUTOKA TAASISI ZA UMMA
yaani makala yote RAIS MAGUFULI APOKEA GAWIO LA TSH BILIONI 736 KUTOKA TAASISI ZA UMMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS MAGUFULI APOKEA GAWIO LA TSH BILIONI 736 KUTOKA TAASISI ZA UMMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/rais-magufuli-apokea-gawio-la-tsh.html
0 Response to "RAIS MAGUFULI APOKEA GAWIO LA TSH BILIONI 736 KUTOKA TAASISI ZA UMMA"
Post a Comment