title : Wanawake Milioni 2.6 Kunufaika na Mradi wa ‘50 Million Women Speak Project’
kiungo : Wanawake Milioni 2.6 Kunufaika na Mradi wa ‘50 Million Women Speak Project’
Wanawake Milioni 2.6 Kunufaika na Mradi wa ‘50 Million Women Speak Project’
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Takribani wanawake milioni 2.6 wanategemea kunufaika na mradi ujulikanao kama 50 Million Women Speak Project’ unaolenga kuwawezesha wanawake kupata taarifa za kiuchumi kupitia mtandao wa mawasiliano.
Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bw. Julius Mbilinyi alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa Kitaifa wa masuala ya maendeleo ya wanawake nchini.
Bw. Mbilinyi amesema kuwa takwimu za Hali ya Afya na Demografia za mwaka 2015 zinaonesha asilimia 51 ya Watanzania ni wanawake ambao kati ya wanawake hao, asilimia 70 wanajihusisha na shughuli za kilimo na ujasiriamali hivyo mradi huo utatumika kusaidia kuimarisha shughuli zao.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bw. Julius Mbilinyi akifungua kikao cha wadau wa Kitaifa wa masuala ya maendeleo ya wanawake nchini kilichofanyika jijini Dodoma.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Sekta ya Jamii kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mary Makoffu na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana na Uwezeshaji Kiuchumi, Esther Riwa.
Msimamizi wa Mradi huo kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Wilson Muyenzi akitoa mada katika kikao cha wadau wa Kitaifa wa masuala ya maendeleo ya wanawake nchini kilichofanyika jijini Dodoma.
Hivyo makala Wanawake Milioni 2.6 Kunufaika na Mradi wa ‘50 Million Women Speak Project’
yaani makala yote Wanawake Milioni 2.6 Kunufaika na Mradi wa ‘50 Million Women Speak Project’ Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wanawake Milioni 2.6 Kunufaika na Mradi wa ‘50 Million Women Speak Project’ mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/wanawake-milioni-26-kunufaika-na-mradi.html
0 Response to "Wanawake Milioni 2.6 Kunufaika na Mradi wa ‘50 Million Women Speak Project’"
Post a Comment