Naibu Waziri Madini : wamiliki mgodi wa Nyakavangala wakamatwe

Naibu Waziri Madini : wamiliki mgodi wa Nyakavangala wakamatwe - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Naibu Waziri Madini : wamiliki mgodi wa Nyakavangala wakamatwe, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Naibu Waziri Madini : wamiliki mgodi wa Nyakavangala wakamatwe
kiungo : Naibu Waziri Madini : wamiliki mgodi wa Nyakavangala wakamatwe

soma pia


Naibu Waziri Madini : wamiliki mgodi wa Nyakavangala wakamatwe

 
 
Na Asteria Muhozya, Iringa
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ameamuru kukamatwa kwa Wamiliki wa mgodi wa Nyakavangala unaomilikiwa na  Thomas Masuka and Partners kufuatia wamiliki hao kutofautiana juu ya taarifa waliyoiwasilisha kwa Naibu Waziri kuhusu namna mgodi huo unavyoendeshwa ikiwemo ulipaji wa kodi na mrabaha wa serikali.

Aidha, Naibu waziri amewataka wamiliki hao kutoa maelezo ya kina kuhusu ni lini watalipa kodi zote wanazodaiwa na serikali baada ya kuonekana kuwa mgodi huo unadaiwa zaidi ya shilingi milioni 128 za mrabaha ambazo imedaiwa kuwa, wapo baadhi ya wamiliki ambao wamekuwa wakikusanya fedha hizo lakini zimekuwa hazilipwi.

Katika ziara yake mkoani humo, Naibu Waziri alisema kuwa pamoja na kujionea shughuli za uchimbaji katika migodi ya dhahabu ya Ulata na Nyakavangala, amebaini ukwepaji mkubwa wa kodi pamoja na mrabaha wa serikali.

Pia, amemtaka Afisa Madini kutoa maelekezo ya kina kuhusu suala zima la ulipwaji wa kodi na mrabaha wa serikali, huku akiagiza zoezi hilo pia limuhusishe Afisa Msimamizi wa madini aliyekuwepo katika kipindi ambacho fedha hizo hazikulipwa.

“Hatutaki ugomvi hapa kwenye migodi. Tunataka mgodi ufanye kazi. Dhahabu ziuzwe mahali panapoonekana. Hapa naona hesabu za viroba tu. Mnunuzi wa dhahabu hapa ni nani”, alihoji Naibu  Waziri.

Wakati akizungumza na wachimbaji katika mkutano wa hadhara, amewataka wachimbaji hao kuchimba kwa kuzingatia usalama  huku akisisitiza suala la kufuata sheria na taratibu huku akiwataka kutoa taarifa za uhakika kwa wale wote wanaokikuka sheria ikiwemo watoroshaji wa madini huku akisisitiza  utoaji taarifa hizo usiwe wa majungu.

Akitolea ufafanuzi suala la fedha za mrabaha, amesema fedha hizo hazipaswi kuelekezwa katika masuala mengine na wamiliki wa migodi ikiwemo kutumiwa katika huduma za jamii badala yake  zinapaswa kulipwa serikalini.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwataka wamiliki hao kukaa chini na kukubaliana namna ya kulipa kiasi cha fedha ambacho wanadaiwa na serikali huku akimtaka Afisa kutoka Halmashauri anayehusika na masuala ya usimamizi wa fedha kuhakikisha kwamba fedha ambazo mgodi huo ulipaswa kuzilipa kama mrabaha zinapatikana.

Mgodi huo wa Nyakavangala unamilikiwa na Thomas Masuka kwa ushirikiano na wawekezaji wengine wazawa wapatao 20. Wakati akiagiza kukamatwa kwao, wamiliki 8 kati ya 20 ndiyo walikuwa wamehudhuria kikao kati yake na wamiliki hao.

Naibu Waziri Nyongo alitoa agizo hilo Januari 15 wakat akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani humo.


Hivyo makala Naibu Waziri Madini : wamiliki mgodi wa Nyakavangala wakamatwe

yaani makala yote Naibu Waziri Madini : wamiliki mgodi wa Nyakavangala wakamatwe Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Waziri Madini : wamiliki mgodi wa Nyakavangala wakamatwe mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/naibu-waziri-madini-wamiliki-mgodi-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Naibu Waziri Madini : wamiliki mgodi wa Nyakavangala wakamatwe"

Post a Comment