title : Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Kuchochea Uwazi na Uwajibikaji
kiungo : Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Kuchochea Uwazi na Uwajibikaji
Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Kuchochea Uwazi na Uwajibikaji
Frank Mvungi- MAELEZO, Mbeya
Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma katika Mamlaka za Serikali za Mitaa toleo la 10.2 (Epical 10.2 ) umetajwa kuchochea utekelezaji wa dhana ya uwazi, uwajibikaji na utawala bora katika usimamizi wa fedha za umma .
Akisoma hotuba ya Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Bi. Mariam Mtunguja, Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Bi. Paulina Ntigeza amesema kuwa mafunzo ya mfumo wa Epicor 10.2 yatasaidia kuongeza tija katika utendaji kutokana na mfumo huo kuandaliwa mahsusi kuungana na mifumo mingine ili kukidhi matakwa ya maboresho yanayofanywa katika usimamizi wa fedha za umma.
Mafunzo hayo yanawashirikisha wahasibu, maafisa ugavi, na waweka hazina wa mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukw, ns yanaendeshwa na Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), kwa kushirikiana na Serikali ya Marekani kupitia Mradi wa Uimarishwaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3, unaosimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani ( USAID), .
Hivi sasa, Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini zitatumia mfumo mmoja wa uhasibu ujulikanao kama mfumo wa usimamizi wa Fedha za Umma, toleo la 10.2 utakaosaidia kuhakikisha kuna mfanano katika uhasibu,utoaji wa taarifa na usimamizi wa fedha.
“Mafunzo haya yana lengo la kuwajengea uwezo ili muweze kusimamia mapato na matunizi ya fedha za umma kwenye Halmashuri na pia kuwapatia uelewa wa mabadiliko ya msingi yaliyofanyika bila kukwamisha utoaji wa huduma kwa wananchi” Alisisitiza Ntigeza
Akifafanua Bi. Ntigeza amesema kuwa Makatibu Tawala wa Mikoa watahakikisha kuwa kuna matumizi sahihi ya mifumo kuanzia ngazi za vituo vya kutolea huduma kuanzia mkoani hadi ngazi ya Halmashuri zote.
Aliongeza kuwa awali maafisa katika maamlaka za Serikali za walilazimika kupitia mipango na bajeti katika mfumo mmoja, mapato katika mfumio mwingine na matumizi kwenye mfumo mwingine, hivyo kuleta ugumu katika uwajibikaji,ufanisi, na thamani ya fedha katika matumizi ya fedha za Serikali.
Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Bi. Paulina Ntigeza akisisitiza umuhimu wa Mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma wa Epicor toleo la 10.2 kwa wahasibu, waweka hazina, Maafisa Ugavi wa Mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukwa kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi. Mariam Mtunguja leo Jijini Mbeya wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Mkuu wa Timu ya Mifumo kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Bw. Desderi Wengaa akitoa maelezo kuhusu mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma wa Epicor toleo la 10.2 utakavyosaidia kuboresha utendaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa leo Jijini Mbeya wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia hotuba ya Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Bi. Paulina Ntigeza ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma wa Epicor toleo la 10.2 yanayofanyika Jijini Mbeya yakiwashirikisha Wahasibu, Maafisa Ugavi na Waweka Hazina kutoka Mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukwa.
Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Bi. Paulina Ntigeza akifungua mafunzo kuhusu Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma wa Epicor toleo la 10.2 niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi. Mariam Mtunguja leo Jijini Mbeya. Mafunzo hayo yanawashirikisha wahasibu, waweka hazina, maafisa ugavi wa Mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukwa .
Mkuu wa Timu ya Mifumo kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Bw. Desderi Wengaa akiagana na Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Bi. Paulina Ntigeza ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi. Mariam Mtunguja leo Jijini Mbeya katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma wa Epicor toleo la 10.2 kwa wahasibu, waweka hazina, Maafisa Ugavi wa Mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukwa
Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Bi. Paulina Ntigeza akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo kuhusu Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma wa Epicor toleo la 10.2 yalishirikisha wahasibu, waweka hazina, Maafisa Ugavi wa Mikoa ya Mbeya, Songwe leo Jijini Mbeya. (Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Mbeya)
Hivyo makala Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Kuchochea Uwazi na Uwajibikaji
yaani makala yote Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Kuchochea Uwazi na Uwajibikaji Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Kuchochea Uwazi na Uwajibikaji mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/mfumo-wa-usimamizi-wa-fedha-za-umma.html
0 Response to "Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Kuchochea Uwazi na Uwajibikaji"
Post a Comment